Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Novemba 22, 2024 Local time: 18:34

Russia yashutumiwa kuulenga mfumo wa umeme na miundombinu ya kiraia Ukraine


Mlinzi yuko mbele ya kinu cha nishati ya nyuklia cha Zaporizhzhia, huku majeshi ya Russia yakiendelea kuishambulia Ukraine, Sept. 11, 2022.
Mlinzi yuko mbele ya kinu cha nishati ya nyuklia cha Zaporizhzhia, huku majeshi ya Russia yakiendelea kuishambulia Ukraine, Sept. 11, 2022.

Maafisa wa Ukraine wameishutumu Russia kwa kuulenga  mfumo wa umeme wa Ukraine na miundombinu mingine ya kiraia baada ya majeshi ya Ukraine kupata mafanikio  katika kujibu mashambulizi huko kaskazini mashariki mwa nchi hiyo.

“Giza limetanda katika mikoa ya Kharkiv na Donetsk, na sehemu ya mikoa ya Zaporizhzhia, Dnipropetrovsk na Sumy,” Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskyy aliandika katika ujumbe wa Twitter Jumapili usiku. “Hakuna vituo vya kijeshi, lengo lao ni kuwanyima watu huduma ya umeme na joto,”

Jeshi la Ukraine limedai kupata mafanikio kadhaa katika siku za karibuni kwenye mkoa wa Kharkiv, ikiwemo kuukamata tena mji wa Izyum ambao majeshi ya Russia yaliutumia kama kituo muhimu cha kijeshi na usambazaji wa mahitaji.

Mkuu wa Jeshi la Ukraine, Jenerali Valerii Zaluzhnyi, alisema kuwa Ukraine imeweza kukamata tena takriban kilomita 3,000 za eneo la mraba lililokuwa mikononi mwa majeshi ya Moscow tangu mwanzoni mwa Septemba. Amesema majeshi ya Ukraine hivi sasa yako kilomita 50 kutoka mpaka na Russia.

Kupiga hatua katika uwanja wa mapambano kumeipa Ukraine mafanikio makubwa sana mapema katika vita hivi ilipoweza kuzuia jaribio la Russia kuukamata mji mkuu, Kyiv. Shambulizi la Ukraine katika mkoa wa Kharkiv limeonekana kuishangaza Moscow, ambayo ilikuwa imehamisha sehemu kubwa ya majeshi yake kutoka eneo hilo kuelekea kusini, ambako Kyiv ilikuwa imetangaza waziwazi kuwa itajibu mashambulizi.

Waziri wa Ulinzi wa Russia, akijibu mafanikio ya Ukraine, alisema Jumamosi kuondolewa kwa majeshi kutoka Izyum na maeneo mengine katika mkoa wa Kharkiv kulikua na azma ya kuimarisha majeshi ya Russia katika mkoa wa jirani wa Donetsk ulioko kusini.

XS
SM
MD
LG