Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Novemba 06, 2024 Local time: 02:52

Russia inaandaa pigo kubwa la nishati kwa ulaya;asema Zelenskiy


Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskiy wakati akitoa hotuba yake ya kila siku kwa njia ya video
Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskiy wakati akitoa hotuba yake ya kila siku kwa njia ya video

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskiy ameiambia ulaya kutarajia msimu mgumu wa baridi kwani shambulizi la Russia dhidi ya nchi yake linasababisha kupunguzwa kwa usafirishaji wa mafuta pamoja na gesi na Moscow.

Zelenskiy alikuwa akizungumza Jumamosi usiku baada ya Moscow kufunga bomba kuu linalosambaza gesi ya Russia kwenda barani humo. Russia inaandaa pigo kubwa la nishati kwa watu wote wa ulaya kwa msimu huu wa baridi kali alisema katika hotuba yake ya kila siku kwa njia ya video.

Moscow imetaja vikwazo vya nchi za magharibi vilivyowekwa kutokana na uvamizi wake nchini Ukraine na masuala ya kiufundi kutokana na usumbufu wa nishati. Nchi za ulaya ambazo zinaiunga mkono serikali ya Kyiv kwa kutoa msaada wa kidiplomasia na kijeshi zimeishutumu Russia kwa kutumia usambazaji wake wa gesi kama silaha.

Baadhi ya wachambuzi wanasema uhaba wa gesi na kuongezeka kwa gharama ya maisha wakati wa msimu wa baridi kali unapokaribia kuna hatari ya kuondoa uungwaji mkono wa nchi za magharibi kwa Kyiv wakati serikali zikijaribu kukabiliana na watu waliochoshwa.

XS
SM
MD
LG