Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Desemba 27, 2024 Local time: 01:34

Mapambano ya nishati kati ya Russia na nchi za Magharibi yaongezeka


FILE - Mabomba ya kusafirisha gesi ya Nord Stream 1 huko Lubmin, Germany, March 8, 2022.
FILE - Mabomba ya kusafirisha gesi ya Nord Stream 1 huko Lubmin, Germany, March 8, 2022.

Mapambano ya nishati kati ya Russia na nchi za Magharibi juu ya vita nchini Ukraine yameongezeka Ijumaa huku Moscow ikichelewesha kufungua tena bomba kuu la mafuta kwenda Ujerumani na Kundi la mataifa saba ikitangaza  bei ya mafuta ya Russia yanayouzwa nje ya nchi.

Kampuni kubwa ya nishati ya Gazprom ya Russia imesema haikuweza kusafirisha gesi asilia kwenda Ujerumani, saa kadhaa kabla ya muda uliopangwa kuanza tena usafrishaji kupitia pomba la mafuta la Nord Stream 1. Russia imelaumu tatizo la kiufundi kwenye bomba hilo la kwa hatua iliyochukuliwa, na huenda ikasababisha hali mbaya zaidi ya mgogoro wa nishati Ulaya.

Msemaji wa Tume ya Ulaya Eric Mamer alisema Ijumaa kupitia ujumbe wa Twitter kuwa Gazprom ilifanya hivyo kwa “kisingizio cha uongo” kufunga bomba la mafuta.

Kampuni inayotengeneza mashine za umeme Siemens Energy ilisema Ijumaa kuwa hakukuwa na sababu za kiufundi kusimamisha usafirishaji wa gesi asilia.

Moscow imelaumu vikwazo vya Magharibi ambavyo vilianza kuonyesha athari zake baada ya Russia kuivamia Ukraine na hivyo kudumaza ukarabati wa bomba la gesi.

Ulaya inaishutumu Russia kwa kutumia gesi yake kama silaha ya kulipiza kisasi dhidi ya vikwazo vilivyowekwa na Ulaya.

Ijumaa, mawaziri wa fedha kutoka nchini wanachama wa G-7 walisema watafanya juhudi za haraka kutekeleza udhibiti wa bei ya mafuta yanayouzwa nje ya nchi na Russia.

Mawaziri hao wa G-7 kutoka Uingereza, Canada, Ufaransa, Ujerumani, Italia, Japan na Marekani walisema kiwango cha bei kitachowekwa kitaangaliwa baadae “kulingana na maelezo mbali mbali ya kiufundi."

XS
SM
MD
LG