Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Desemba 27, 2024 Local time: 17:39

Russia yatoa gesi kidogo kwa Umoja wa Ulaya


Russia - Vladimir Putin
Russia - Vladimir Putin

Russia imetoa gesi kidogo kwa Ulaya Jumatano huku mivutano ya nishati ikiendelea kuongezeka  kati ya Moscow na Umoja wa Ulaya ambayo itafanya iwe vigumu, na gharama kubwa kwa umoja  huo kujaza hifadhi kabla ya msimu wa baridi kali unaohitaji kuitumia  kwa ajili ya joto.

Punguzo la usambazaji wa gesi liligusiwa na Gazprom mapema wiki hii limepunguza uwezo wa bomba la mafuta la Nord stream 1 kwa theluthi tano, njia kuu ya kupitisha gesi ya Russia kwenda Ulaya.

Nord stream 1 inachangia theluthi moja ya mauzo yote ya gesi nje ya Russia barani ulaya.

Jumanne nchi za Umoja wa Ulaya ziliidhinisha mpango wa dharura wa kupunguza mahitaji ya gesi baada ya kufikia makubaliano na ya kupunguza viwango katika baadhi ya nchi zikitaratijia matumizi ya chini yatapunguza athari endapo Moscow itasimamisha usambazaji wa gesi kabisa.

Hata hivyo mpango huo ulizusha wasiwasi kwamba nchi zinaweza kushindwa kufikia malengo kujaza tena hifadhi zake na kuwafanya raia wake kuwa na joto majira ya baridi kali.

XS
SM
MD
LG