Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Desemba 28, 2024 Local time: 09:47

Usafirishaji wa nafaka ya Ukraine kuanza tena hivi karibuni-UN


Katibu mkuu wa UN Antonio Guterres, waziri wa miundombinu wa Ukraine Oleksandr Kubrakov , Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan na waziri wa ulinzi wa Uturuki Hulusi Akar wakihudhuria hafla ya utiaji wa saini mjini Istanbul, Julai 22, 2022. Picha ya Reuters
Katibu mkuu wa UN Antonio Guterres, waziri wa miundombinu wa Ukraine Oleksandr Kubrakov , Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan na waziri wa ulinzi wa Uturuki Hulusi Akar wakihudhuria hafla ya utiaji wa saini mjini Istanbul, Julai 22, 2022. Picha ya Reuters

Umoja wa mataifa Jumatatu umesema kwamba usafirishaji wa nafaka ya Ukraine utaanza tena ndani ya siku chache licha ya kuwa umelaani mashambulizi ya makombora ya Russia katika bahari nyeusi ya Odesa ndani ya saa chache baada ya kukubali kuanzishwa kwa usafirishaji wa shehena za chakula.

Usafirishaji wa nafaka hiyo utafanyika kutoka Odesa na bandari nyingine mbili za bahari ya Black Sea, ambazo ni Chernomorsk na Yuzhny, msemaji wa Umoja wa mataifa Farhan Haq amesema, na kuongeza kwamba “tunataka kuhakikisha kuwa mazingira yote ni bora kwa ajili ya safari salama za meli.”

“Chochote ambacho hakiambatani na hilo, bila shaka hakisaidii kufanikisha mpango huu,” Haq amesema, huku akisisitiza msimamo wa katibu mkuu Antonio Guterres kwa kuilaani Russia kwa shambulio lake la kombora dhidi ya bandari ya Odesa Jumamosi.

Hata hivyo, waziri wa mambo ya nje wa Russia Sergey Lavrov alidai kwamba “ hakuna chochote katika ahadi za usafirishaji wa nafaka ambazo Russia ilitia saini mjini Istanbul ambacho kitatuzuia kuendelea na operesheni yetu maalum ya kijeshi, kuharibu miundombinu ya kijeshi na vituo vingine vya kijeshi.

Russia Jumatatu imesema mashambulizi yake ya makombora kwenye mitambo ya kijeshi huko Odesa hayatoathiri makubaliano ya kuanza tena usafirishaji wa nafaka.

XS
SM
MD
LG