Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Desemba 25, 2024 Local time: 09:31

Kupanda kwa bei ya nishati ulimwenguni kwatikisa uchumi Afrika


Africa map
Africa map

Waafrika wanahisi maumivu ya kupanda kwa bei za nishati ulimwenguni, wanasema wachambuzi, hata kwa nchi kama vile Nigeria na Angola ambazo wauzaji wakubwa wa mafuta ghafi duniani.

Wakati mataifa kadhaa yanayozalisha mafuta yanaona ongezeko la mapato – hasa tangu uvamizi wa Russia huko Ukraine Februari 24 – sehemu kubwa ya bara hilo halina uwezo wa kusafisha mafuta, na kuzilazimisha nchi kulipa bei kubwa kwa kuagiza mafuta na bidhaa nyingine za petroli kutoka Asia na Ulaya.

Bara hilo linaathiriwa zaidi na ongezeko la gharama za gesi ya asili, kiini katika mbolea ambayo inatumiwa katika uzalishaji chakula.

Huku mishahara ikiwa imesimama, zaidi ya theluthi mbili ya waafrika wanahisi shinikizo kubwa la kupanda kwa bei za bidhaa, alisema Franklin Cudjoe, rais muanzilishi wa kituo cha Imani cha Sera na Elimu chenye makao yake nchini Ghana.

“Bara hilo limeathiriwa kwasababu ya kutegemea kwa kiasi kikubwa kwa wasambazaji mafuta wa nje, kwa vile si nchi nyingi za kiafrika zina zalisha bidhaa hiyo,” Cudjoe ameiambia VOA.

Bei zimepanda kwenye soko la dunia la mafuta baada ya Ukraine kuvamiwa na kuchochea wimbi la vikwazo vya kimataifa dhidi ya Russia, moja ya muuzaji mkubwa sana wa mafuta ghafi duniani. Bei zilipanda kwa muda mfupi kwa zaidi ya $120 kwa pipa mwezi kabla ya kushuka hadi #103 kwa pipa siku ya Ijumaa.

Bei ya mafuta ya rejareja yapanda Marekani.Photo by MANDEL NGAN / AFP)
Bei ya mafuta ya rejareja yapanda Marekani.Photo by MANDEL NGAN / AFP)

Ongezeko la bei za nishati linasaidia mfumoko wa bei za mafuta kote barani Afrika. Nchini Ghana, kwa mfano, bei ya mafuta kwa jumla kwa mnunuzi ilipanda na kufikia 15.7% kwa mwaka mwezi Februari ukilinganisha na 13% mwezi Januari, idara ya Hudma za Takwimu katika nchi zilisema wiki iliyopita.

Nchini Zimbabwe, bei zilipanda kwa kiwango cha juu. Kwenye duka la vyakula la TM katika mji mkuu Harare, kreti ya yenye mayai 30 iligharimu $6.70 siku ya Jumanne na kiasi cha $7.81 siku ya Jumatano. Bei ya mkate ilipanda kutoka $1.49 mpaka $1.84; kilo ya nyama, ilipanda kutoka $3.35 mpaka $5.22.

Gharama za mafuta nazo pia zilipanda. Mjini Harare, bei ya lita moja ya mafuta ilipanda kutoka $1.41 mpaka $1.69 kutoka Jumanne hadi Jumatano.

Kupanda kwa bei za vyakula ilikuwa ndiyo kiini kikuu kwa mfumuko wa bei kwa ununuzi nchini Misri. Ulipanda kwa 8.8% mwezi Februari – ikiwa ni ongezeko kubwa sana kwa kipindi cha karibu miaka mitatu, kwa mujibu wa idara ya takwimu, CAPMAS.

Cudjoe alisema ilikuwa muhimu kwa serikali na taasisi za kikanda kama vile Umoja wa Afrika kujenza ulinzi ili kuwasaidia wanunuzi wakati wa kipindi kisichokuwa na uhakika cha uchumi.

“Hata kama ina maana ya kujenga ulinzi katika misingi ya chakula,” alisema Cudjoe, akiongezea, “naweza kufikiria jinsi Nigeria, kama ingekuwa na njia yake, huenda wangeuza chakula kwa nchi nyingi kwa viwango vya chini hivi sasa.”

“Lazima kuwepo na uharaka wa kujijengea ulinzi, ufadhili ambao huenda ukawasaidia kujihimili – walau kutuzuia kuangamizwa kabisa na hali hii ya kutokuwa na uhakika hapa duniani.”

Chibamba Kanyama, mchumi katika mji mkuu wa Zambia, Lusaka, alisema kusitisha kodi za mafuta huenda ikawa “ni jambo jema sana kufanya hivi sasa na hali ilivyo” kuwasaidia wateja na viwanda.

“Serikali za kiafrika lazima zibuni njia za kujibu,” alisema. “Ni uchaguzi wa iwapo kupunguza kodi ili kushusha bei au kuendeleza bei katika viwango vile vile na kutumia mapato kutoa ruzuku kwa jamii ambazo ziko katika mazingira hatarishi.”

Lakini Kanyama pia anapendekeza kwamba mzozo wa kisiasa kijiografia unaihusisha Russia na Ukraine wote ni wauzaji wakubwa wa nafaka kwa Afrika – huenda wakafungua fursa kwa wazalishaji wa kiafrika.

“Nchi ambazo ni wasambazaji kama Afrika Kusini, zenye mifumo madhubuti na yenye teknolojia ya juu, huenda yakafungua dirisha la usafirishaji bidhaa kama vile ngano na bidhaa nyingine ili kujaza mianya iliyoachwa wazi na Russia na Ukraine,” Kanyama amesema.

Kanyama pia amesema uungaji mkono wa jumuiya ya kimataifa – kwa mfano, katika mpango wa ahueni ya madeni kwa baadhi ya nchi za Afrika itakuwa ni jambo jema.

Alielezea kwamba kundi la mataifa 20 ambalo linajumuisha mataifa saba yaliyoendelea kiviwanda, baadhi ya nchi zenye nguvu au ambazo uchumi wake unakua kwa haraka, na Umoja wa Ulaya, “zinajaribu kutoka aina fulani ya ahueni ya madeni.”

“Baadhi ya nchi nyingine, kama vile Zambia, zinapitia kipindi cha mchakato wa kushughulikia madeni yake na pia program ya IMF, kwangu mimi, hii ni njia pekee ya kututoa katika mgogoro,” Kanyama aliongezea.

XS
SM
MD
LG