Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Novemba 05, 2024 Local time: 15:35

Afrika: China yakabiliwa na changamoto ya uchimbaji madini ya nickel hadi cobalt


Uchimbaji wa madini umegundua dhahabu, zinc, nickel na aina nyingine za madini huko eneo la Meiganga, Cameroon. (M. Kindzeka/VOA)
Uchimbaji wa madini umegundua dhahabu, zinc, nickel na aina nyingine za madini huko eneo la Meiganga, Cameroon. (M. Kindzeka/VOA)

Kampuni kubwa ya Kichina ya nikeli ya Tsingshan Holding Group ilitabiri bei za nikeli zitashuka, lakini badala yake, uvamizi wa Russia nchini Ukraine umeifanya bidhaa hiyo kupanda bei kwa kiwango kikubwa sana wiki iliyopita...

Ni chuma kinachopatikana katika bidhaa zinazotumiwa na watu kote duniani, bila ya kufikiria, kila siku.

Iwe ni kwenye simu ya mkononi au wakati unakwenda kazini ukiwa ndani ya gari inayotumia umeme, nikeli ni kifaa muhimu katika vifaa hivyo vya teknolojia ya hali ya juu.

Hivi sasa – ni muhimu katika betri – kinatikisa masoko na kampuni moja ya Kichina inakabiliwa na hasara ya mabilioni ya dola.

Kampuni kubwa ya Kichina ya nikeli ya Tsingshan Holding Group ilitabiri bei za nikeli zitashuka, lakini badala yake, uvamizi wa Russia nchini Ukraine umeifanya bidhaa hiyo kupanda bei kwa kiwango kikubwa sana wiki iliyopita, na kusukumwa na wasi wasi kuhusu mtikisiko wa kampuni ya Russia ya Nornickle, moja ya wasambazaji wakubwa sana duniani.

Wakati mmoja bei zilipanda kwa 250%, na kuchochea Soko la Hisa ya Chuma Uingereza (LME) kusimamisha biashara zake. Bei zilianguka wakati soko lilipofunguliwa tena Jumatano, lakini hali ilibadilika haraka sana na kusimamishwa tena kwa biashara, akisema walikuwa wakichunguza kosa hilo la kiufundi.

FILE PHOTO: Wafanyabiashara wakiwa katika ofisi za London Metal Exchange, London, Uingereza, September 27, 2018. REUTERS/Simon Dawson/File Photo
FILE PHOTO: Wafanyabiashara wakiwa katika ofisi za London Metal Exchange, London, Uingereza, September 27, 2018. REUTERS/Simon Dawson/File Photo

Mtikisiko wa soko imekuwa ni habari mbaya kwa Tshingshan, msambazaji mkubwa sana wa nikeli, kama ilivyo kwa makampuni mengi ya madini ya China yamekuwa na maslahi makubwa barani Afrika – hasa nchini Zimbabwe yenye utajiri wa nikeli.

Kampuni hiyo yenye makao yake Wenzhou, imerekodi mapato ya dola bilioni 19 mwaka 2021, inajenga kiwanda kikubwa cha madini chenye gharama ya dola bilioni moja nchini Zimbabwe chenye uwezo wa kuzalisha tani milioni 1.2.

Akiulizwa na VOA siku ya Jumatano kama ana wasi wasi na kampuni hiyo kupata hasara na hivyo kusitisha au kupunguza maendeleo yao katika nchi yake, Waziri wa Habari wa Zimbabwe, Monica Mutsvangwa alisisitiza.

Waziri wa Habari wa Zimbabwe, Monica Mutsvangwa. (Columbus Mavhunga/VOA))
Waziri wa Habari wa Zimbabwe, Monica Mutsvangwa. (Columbus Mavhunga/VOA))

“Hapana, siyo hivyo kabisa,” alisema. “Mradi unasonga mbele kama ilivyopangwa.”

Mutsvangwa alisisitiza kwamba miradi ya Zimbabwe, “inafadhiliwa na mtaji muhimu uliotengwa katika bajeti kwa ajili ya biashara ya chuma… kwa hakika siyo Soko la Hisa ya Chuma Uingereza, LME, linalokopesha kuwekeza.”

Hata hivyo, Christian Geraud Neema Byamungu, mchambuzi wa sera na madini na mhariri wa mradi wa China Afrika, alisema hasara waliyopata Tsingshan “inaweza kuchelewesha operesheni zake nchini Zimbabwe kwa muda mfupi.”

“Hii itakuwa habari mbaya kwa Zimbabwe, ambapo matarajio yako juu kwa mradi huu,” aliongezea. “Katika awamu hii hali ambayo tunaweza kuifikiria ni kwamba itaturudisha nyuma na si tatizo la muda mrefu kwa vile hatujapima matokeo halisi ya hasara.”

Barua pepe kutoka makao makuu ya Tsingshan ambazo VOA ilituma hazikujibiwa, wakati Benson Xu, mkurugenzi mtendaji wa kampuni tanzu nchini Zimbabwe, hakujibu maombi ya mara kwa mara kutafuta maoni. Barua pepe kwa ubalozi wa China mjini Harare nayo pia haikujibiwa.

Hata hivyo, katika taarifa fupi iliyobandikwa kwenye tovuti ya kampuni Jumanne, kundi hilo lilisema limefikia “makubaliano na wakopeshaji kadhaa kuhusu makubaliano ya kifedha.” Jumatano, Reuters iliripoti kuwa kampuni kubwa ilifikia makubaliano na makampuni mawili ambayo hayakutajwa kufunga baadhi ya nafasi ambazo inazishikilia.

Tsingshan huenda ikaterereka kutoka na mzozo wa nikeli, lakini Muchadeyi Masunda, mwenyekiti wa kampuni Bindula Nickel Corpo yenye makao yake nchini Zimbabwe, aliiambia VOA kuwa anahisi “wanahamasa” na wanamatumaini BNC itakuja “kupata baadhi ya maslahi.”

“Tumekuwa tukiangalia kwa utashi mkubwa na wasi wasi kwa maendeleo kwenye LME hasa tukiangalia bei za nikeli, kufuatia uvamizi wa Russia huko Ukraine,” alisema Masunda.

Kwanza alisema, “tunasugua mikono yetu pamoja tukifurahia tutawapata,” wakati bei za bidhaa zikipanda. Lakini mambo yamesogea haraka kwa hiyo kampuni hivi sasa ina wajibu na kuchochea miradi kadhaa, pengine hata kurejesha madini ambayo hayatumiki, alisema.

Masunda, ambaye alisema baadhi ya bidhaa za BNC ‘ kwa hakika zinaishia China,” hatazungumza kuhusu Tsingshan.

Madini ya Cobalt

Kilichotokea kwa bei za nikeli hivi sasa kinategemea kwa kiasi kikubwa “kile ambacho kitatokea kwa vikwazo kwa Russia,” alisema Geoggrey Sambrook, ambaye alikuwa akifanya biashara na LME kwa miongo kadhaa.

Wateja – kimsingi wazalishaji wa chuma na watengenezaji betri – watakuwa na wasi wasi kuhusu mfumo wa ugavi,” ameiambia VOA, akielezea kwamba huenda ikashawishi makampuni tayari kuangalia utengenezaji betri ambao hautumii madini ya gharama au cobalt.

Madini ya Cobalt yamethibitika kuwa ni mtihani kwa kampuni nyingine kubwa ya China yenye shughuli zake huko barani Afrika.

Vipande vya madini ya cobalt yakitayarishwa kwa ajili ya kusafirisha nje ya nchi, na zaidi ni China katika kiwanda cha Lubumbashi, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, on Feb. 16, 2018. (Photo by SAMIR TOUNSI / AFP).
Vipande vya madini ya cobalt yakitayarishwa kwa ajili ya kusafirisha nje ya nchi, na zaidi ni China katika kiwanda cha Lubumbashi, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, on Feb. 16, 2018. (Photo by SAMIR TOUNSI / AFP).

Mapema mwezi huu, mahakama moja huko Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo, chanzo kikubwa sana cha madini ya cobalt, iliiamuru kampuni kubwa ya China ya Molybdnenum kusitisha operesheni zake kubwa kwenye machimbo ya Tenke Fungurume ya cobalt na shaba mpaka mzozo wa wana hisa utakaposuluhishwa. Rais wa Congo, Felix Tshisekedi aliapa mwaka jana “kusafisha” sekta ya madini na kutathmini makubaliano ya “miundo mbinu kwa madini” kati ya serikali ya awali na Wachina.

Wakati maamuzi ya mahakama kwa China Moly huenda yakawa ni adhabu ambayo si kali kwa kampuni ya Kichina, mchambuzi Neema alisema “Maslahi ya wachina nchini huko bado ni imara.”

XS
SM
MD
LG