Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Novemba 22, 2024 Local time: 23:12

Wakazi karibu na kiwanda cha nyuklia cha Ukraine washauriwa kukimbilia usalama


Kiwanda cha nyuklia cha Zaporizhzhia, Ukraine
Kiwanda cha nyuklia cha Zaporizhzhia, Ukraine

Ukraine Jumatano imeomba wakazi waliyoko kwenye maeneo yanayokaliwa na Russia karibu na kiwanda cha nyuklia cha Zaporizhzhia, kuondoka mara moja kwa ajili ya usalama wao.

Taarifa hiyo imetolewa na naibu waziri mkuu wa Ukraine Iryna Vereschuk kupitia ujumbe wa Telegram. Kwenye ujumbe tofauti wa Telegram, meya wa mji wa Enerhodar ambako kiwanda hicho kinapatika, na aliyeko uhamishoni, amesema kwamba kimeshambuliwa na Russia, na kwamba umeme umekatika mjini humo.

Kwa wiki kadhaa sasa , Ukraine na Russia wamekuwa wakilaumiana kutokana na mashambulizi ya makombora kwenye kiwanda hicho ambacho ni kikubwa zaidi cha nyuklia barani Ulaya, hali inayotishia kutokea kwa mkasa sawa na ule wa kiwanda cha Chernobyl mwaka wa 1986 nchini humo.

Jumanne mkuu wa idara ya kimataifa ya nishati ya atomic, Rafael Grossi alisema kwamba mashambulizi dhidi ya kiwanda hicho hayakubaliki kamwe, wakati akiomba kutengwa kwa eneo lisilo ruhusiwa silaha karibu nacho. Moscow wala Kyiv hawajasema lolote kutokana na ombi hilo, wakisema kwamba wanahitaji muda zaidi ili kutadhmini hali ilivyo.

XS
SM
MD
LG