Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Novemba 22, 2024 Local time: 18:46

Ukraine: Mtambo wa sita na wa mwisho wa kuzalisha umeme Kituo cha Zaporizhzhia wazimwa


Kituo cha umeme cha kinu cha nishati ya nyuklia cha Zaporizhzhia.
Kituo cha umeme cha kinu cha nishati ya nyuklia cha Zaporizhzhia.

Ukraine ilisema Jumapili mtambo wa sita na wa mwisho wa  kuzalisha umeme  katika kinu cha nishati ya nyuklia cha Zaporizhzhia kinachodhibitiwa na Russia huko kusini mwa nchi hiyo kilikuwa hakizalishi tena umeme.

“Leo, Septemba 11, 2022, usiku, saa tisa na dakika 41 kwa saa za Ukraine (saa kumi na dakika 41 Afrika Mashariki), mtambo Na 6 wa ZNPP ulizimwa kwenye gridi ya umeme. Maandalizi yako njiani kwa ajili ya kuupoza na kuuweka katika hali iliyo baridi,” shirika la taifa la nyuklia Energoatom limesema katika taarifa yake.

Ukraine na washirika wake walikuwa na wasiwasi zaidi kuhusu usalama wa kuendesha kituo hicho cha Zaporizhzhia – kikubwa sana Ulaya – na mapigano ya karibuni katika eneo hilo yameongeza wasiwasi na khofu ya kutokea ajali mbaya sana.

Taasisi ya uangalizi wa nguvu za atomiki ya Umoja wa Mataifa ilionya mapema kuwa giza katika mji ulio karibu wa Energodar “ulisababisha operesheni zake kutokuwa salama” katika kituo hicho cha nyuklia.

Wataalam wa Shirika la Nguvu za Atomiki la Kimataifa, IAEA, walipotembelea Kinu cha Nishati ya Nyuklia cha Zaporizhzhia.
Wataalam wa Shirika la Nguvu za Atomiki la Kimataifa, IAEA, walipotembelea Kinu cha Nishati ya Nyuklia cha Zaporizhzhia.

Energoatom imesema Jumapili kuwa kuzimwa kwake katika hali ya ubaridi “ndio hali salama zaidi” kwa kinu hicho.

Energoatom ilisema kuwa mtambo wa sita ulikuwa unazalisha umeme kwa ajili ya kinu cha umeme chenyewe kwa siku tatu na uamuzi wa kusitisha operesheni zake umekuja wakati umeme wa nje ulikuwa umerejeshwa katika kituo hicho.

“Iwapo kutatokea tena uharibifu katika njia za kusambaza umeme zilizounganishwa na mtambo huo kwenda katika mfumo wa umeme – hatari iliyopo bado iko juu mahitaji ya ndani ya kituo hicho cha umeme yatazalishwa na majenereta ya dizeli,” taarifa ilitahadharisha.

Energoatom katika taarifa yake kwa mara nyingine tena imetaka kuwekwa kwa eneo ambalo si ruhusu kuwepo kwa harakati za kijeshi kuzunguka kinu hicho cha umeme, ikisema njia pekee ni kuhakikisha usalama wa kinu hicho.

XS
SM
MD
LG