Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Desemba 27, 2024 Local time: 01:34

Putin anasema anataka kujadili makubaliano yanayoruhusu usafirishaji nafaka


Rais wa Russia Vladmir Putin
Rais wa Russia Vladmir Putin

Rais Vladmir Putin wa Russia amesema Jumatano kwamba anataka kujadili kufungua tena makubaliano yaliyosimamiwa na Umoja wa Mataifa ambayo yanairuhusu Ukraine kusafirisha nafaka zake kupitia Black Sea baada ya kuishutumu Kyiv na nchi za magharibi kwa kuitumia hatua hiyo kuzidanganya nchi zinazoendelea na Russia.

Ukosoaji wa Putin ambao ulidai kwamba makubaliano hayo yalikuwa yakusafirisha nafaka, mbolea, na vyakula vingine kwa Umoja wa ulaya na uturuki kwa gharama ya nchi maskini, kuna uwezekano mkubwa wa hofu kuongeeka kwamba makubaliano hayo yanaweza kuvurugika ikiwa hayawezi kujadiliwa upya kwa mafanikio.

Ukraine ambayo bandari zake zilikuwa zimezuiliwa na Russia tangu ilipoivamia mwezi Februari, ilisema masharti ya makubaliano haya yanazingatiwa vikali na hakuna sababu za majadiiano mapya.

Makubaliano hayo yaliyowezeshwa na Umoja wa Mataifa na uturuki mwezi Julai, yaliunda ukanda wa usafirishaji kupitia Black Sea kwa nafaka za Ukraine baada ya Kyiv kupoteza ufikiaji wa njia yake kuu ya kuuza nje wakati Russia ilipoishambulia Ukraine kupitia ardhi, anga na bahari.

XS
SM
MD
LG