Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 08:44

Balozi wa Marekani nchini Russia amaliza muda wake


John Sullivan, balozi wa Marekani nchini Russia
John Sullivan, balozi wa Marekani nchini Russia

Balozi wa Marekani nchini Russia, John Sullivan alimaliza muda wake wa kuwa mwanadiplomasia mkuu wa Marekani mjini Moscow siku ya Jumapili baada ya takribani miaka mitatu kuanzia utawala wa Trump hadi Biden na atastaafu baada ya muda mrefi katika utumishi wa serikali.

Kuondoka kwake ambako kunakuja katikati ya mzozo unaozidi kuwa mkubwa juu ya vita vya Russia nchini Ukraine pamoja na mizozo kuhusu wamarekani waliozuiliwa nchini Russia kulitarajiwa kufika kikomo msimu huu wa FALL kutokana na kwamba alifikia kikomo cha kuhudumu kama balozi wa Marekani.

Lakini pia iliharakishwa kutokana na masuala ya kiafya katika familia, kulingana na watu wanaofahamu suala hilo ambao walizungumza kwa sharti la kutotajwa majina kwa sababu ya usiri wa suala lenyewe. Kuondoka kwa balozi Sullivan kumepangwa na ni sehemu ya mzunguko wa kawaida wa kidiplomasia wizara ya mambo ya nje ya Marekani ilisema. Amehudumu kwa muda wote kama balozi wa Marekani nchini Russia akisimamia moja ya uhusiano mgumu zaidi kati ya nchi hizo mbili duniani katika nyakati ambazo hazijawahi kutokea.

XS
SM
MD
LG