Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Novemba 22, 2024 Local time: 23:46

Waziri Blinken yupo Ukraine na atangaza msaada zaidi


Waziri wa mambo ya nje wa Marekani, Antony Blinken.
Waziri wa mambo ya nje wa Marekani, Antony Blinken.

Waziri wa mambo ya nje wa Marekani, Antony Blinken, yupo Ukraine katika ziara ambayo haikutangazwa ya kuonyesha muendelezo wa Washington kuunga mkono Kyiv, miezi sita baada ya Russia kuivamia Ukraine.

Waziri Blinken Alhamisi ametangaza msaada wa dola bilioni 2.6 kwa Ukraine na mataifa mengine 18 ya kikanda mengi yao yaliyo katika uwezekano wa kukabliwa na uchokozi wa Russia.

Dola bilioni 2.6 zinajumuisha dola milioni 675 kwa ajili ya silaha zaidi, risasi na vifaa vingine kutoka hifadhi ya wizara ya ulinzi ya Marekani.

Kwa kuongeza waziri Blinken, atatangaza wizara ya mambo ya nje kuliomba bunge kuweka utayari wa dola bilioni 2 kwa ajili ya uwekezaji wa muda mrefu chini ya mfungo wa ufadhili wa maajeshi ya mataifa ya nje ili kuongeza usalama wa Ukraine na majirani zake 18.

XS
SM
MD
LG