Mtu aliyewahi kuwa na nguvu aliachia madaraka Aprili 2019 kutokana na shinikizo la jeshi, kufuatia wiki kadhaa za maandamano katika juhudi za kupinga azma yake ya kujaribu kuwania muhula wa tano madarakani.
Baada ya kuachia madaraka, hakujitokeza hadharani aliishi katika makazi yake magharibi mwa Algiers.
Habari za kifo chake Ijumaa jioni zilipokelewa kwa maoni machache katika nchi hiyo ya Afrika Kaskazini, ikionyesha namna gani kuondoka kwake madarakani kulivyopelekea kusahauliwa na umma.
Taarifa iliyotolewa na mrithi wake Abdelmadjid Tebboune, ilielezea Limeeleza historia ya Bouteflika kama mpiganaji wa vita vya kudai uhuru kutoka Ufaransa na kusema bendera zitapeperushwa nusu mlingoti kwa siku tatu kumuenzi..
Lakini katika mitaa ya mji mkuu Algiers, wakazi wengi wameliambia shirika la habari la AFP rais huyo aliyewahi kuwa madarakani kuondoka kwake hakujalishi.
“Ibarikiwe roho yake. Lakini hastahili kupewa heshima yeyote kwa sababu hakufanya chochote kwa ajili ya nchi yake,” alisema muuza mboga huko Rabah.
Malek, mfanyakazi wa shirika la mawasiliano, amesema Bouteflika “hakuweza kuleta mageuzi katika nchi katika kipindi kirefu cha utawala wake”.
Hata watangazaji wa kitaifa hawakuongeza chochote katika habari za kifo chake, na hawakutangaza makala maalum juu ya kumbukumbu ya uongozi wake.
Tovuti ya habari ya Sabqpress imesema mazishi yatafanyika siku ya Jumapili katika makaburi ya El-Alia mashariki mwa mji mkuu ambapo viongozi waliomtangulia na wapigania uhuru wengine wamezikwa.
Hapakuwa na uthibitisho wa mara moja wa mazishi hayo kutoka viongozi wa serikali.