Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Desemba 25, 2024 Local time: 19:18

Rais wa Burundi arejea kusema hatagombea muhula mwengine


Rais wa Burundi Pierre Nkurunziza
Rais wa Burundi Pierre Nkurunziza

Rais wa Burundi amegusia tena kuwa hatagombea awamu nyingine mwaka 2020 katika nchi ya Afrika Mashariki iliyokuwa haina utulivu wa kisiasa.

Rais Pierre Nkurunziza aliwaambia waandishi Alhamisi ana mpango wa kuitisha mkutano mwengine wa waandishi wa habari “kabla ya kumkabidhi madaraka mrithi wake.”

Kunang’ania kwake kugombea tena mwaka 2015 kulipelekea machafuko ya kisiasa yaliyosababisha vifo na madai ya vikundi vya haki za binadamu kulikuwepo udhalilishaji.

Serikali hiyo baadae ilikuwa ni nchi ya kwanza kujiondoa kutoka Mahakama ya Uhalifu wa Kimataifa wakati serikali ikipuuzia ukosoaji juu ya vitendo vyake.

Nkurunziza mwaka 2018 amesema hatogombania tena lakini kauli yake ilipokelewa lakini baadhi ya wafuatiliaji wa siasa za nchi hiyo waliitilia mashaka.

Rais alitoa tamko hilo alipokuwa anazindua katiba mpya ambayo iliongeza muhula wa urais kutoka miaka 5 hadi 7.

Wakati huo Nkurunziza alitangaza kuwa atamuuga mkono yeyote atakaye chaguliwa mwaka 2020 na kuongeza kuwa “mtu anaweza kuhama sehemu moja kwenda nyingine kitandani lakini hawezi kubadilisha kauli yake.”

Rais huyo mwenye umri wa miaka 55 mapema mwezi huu akizungumza na vikosi vya usalama amesema itakuwa ni mara ya mwisho atawatakia heri za sikukuu kama kiongozi wa Burundi. Pia aliwataka waendeleze “umoja na nidhamu” na kuepuka “machafuko.”

XS
SM
MD
LG