Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Januari 14, 2025 Local time: 18:58

Rais-mteule asema anapanga kumteua Kari Lake kuwa mkuu wa VOA


Kari Lake (AFP)
Kari Lake (AFP)

Rais-mteule wa Marekani Donald Trump amesema Jumatano anapanga kumteua Kari Lake, mwanasiasa na mwandishi wa zamani wa Arizona, kuwa mkuu wa taasisi ya kimataifa ya utangazaji  ya Sauti ya Amerika (VOA) inayofadhiliwa na serikali kuu.

Rais-mteule Donald Trump
Rais-mteule Donald Trump

Trump alitangaza katika mtandao wake wa kijamii wa Truth Social kuwa Lake atateuliwa kuwa mkurugenzi wa VOA. Lake ni mshirika wa karibu wa kisiasa wa rais mteule na mtangazaji wa zamani wa kituo cha televisheni cha Fox News huko Phoenix, Arizona.

Amefanya kazi ya uandishi kwa miaka 27 kabla ya kuondoka katika tasnia hiyo mwaka 2021 ili kugombea nafasi ya ugavana huko Arizona.

Katika jaribio la kugombea Useneta lililokuwa limefeli mwaka 2024, Lake alisema Arizona lazima iwe “ndiyo kipimo cha sera za Marekani Kwanza.”

Trump pia aliandika Jumatano kuwa karibuni atamtangaza atakaye ongoza taasisi ya US Agency for Global Media, ijulikanayo kama USAGM, ambayo inasimamia Sauti ya Amerika pamoja na taasisi nyingine za utangazaji zinazofadhiliwa na serikali ya Marekani.

Mtendaji mkuu wa USAGM inayofadhiliwa na umma anahakikisha kuwa taasisi za utangazaji zote zinafikia malengo yake kutayarisha taarifa za kiuandishi zinazo aminika na zilizo sahihi kuzifikia nchi zenye ufinyu wa vyombo huru vya habari.

Mkurugenzi wa sasa wa VOA, Mike Abramowitz, alituma barua pepe kwa wafanyakazi Alhamisi asubuhi akisema kuwa alisoma tangazo kuhusu Lake Jumatano usiku na hakuletewa taarifa zaidi ya zile zilizopachikwa katika mitandao ya kijamii.

Mike Abramowitz
Mike Abramowitz

“Nakaribisha makabidhiano yenye utulivu ya madaraka kwa vyote USAGM na VOA. Nina azma ya kushirikiana na uongozi mpya na kuufuata mchakato” kwa uteuzi wa mkurugenzi wa VOA, aliandika.

Sheria iliyopitishwa mwaka 2020

Afisa Mtendaji Mkuu (CEO) wa USAGM ana madaraka ya kuajiri na kuwafukuza kazi wakuu wa taasisi za mtandao, lakini chini ya mswada uliopitishwa kwa ushirikiano wa vyama vyote viwili Desemba mwaka 2020, mabadiliko ya mkuu wa mtandao unahitaji kura za walio wengi za bodi ya International Broadcasting Advisory Board.

Bodi hiyo ina wajumbe sita waliochaguliwa na rais wanaohudumu kwa mihula mbalimbali, pamoja na Waziri wa Mambo ya Nje. Kazi ya bodi hiyo ni kumshauri CEO kuhakikisha kuwa kiongozi huyo mwanamke au mwanamme anaheshimu uhuru na heshima ya wahariri wa mitandao hiyo na wadhamini, na viwango vya juu kabisa vya uandishi wa habari vinafuatwa.

[[ https://www.ibab.gov/about-us/statute-bylaws-and-functions/ ]]

Katika ujumbe uliopachikwa katika mtandao wa kijamii wa X, Lake alisema ni heshima kwake kufikiriwa kuwa kwenye nafasi hiyo katika VOA.

Alisema kuwa VOA ni chombo cha Habari muhimu cha kimataifa kinachohamasisha “demokrasia na ukweli.”

“Chini ya uongozi wangu, VOA itaendelea kuwa juu katika kazi yake: ikisimulia mafanikio ya Marekani ulimwenguni kote.”

VOA ilijaribu kumfikia Lake kutaka maoni yake kupitia kitengo cha habari cha tovuti ya kampeni yake, lakini mpaka inachapishwa habari hii hakuna majibu.

Matangazo ya VOA kwa wiki yanawafikia wasikilizaji milioni 354 katika lugha 49. Mkurugenzi wake hivi sasa, Abramowitz, ni rais wa zamani wa taasisi ya Freedom House na alikuwa mwandishi wa habari na mhariri wa gazeti la The Washington Post kwa miaka 24.

[[ https://www.voanews.com/a/usagm-names-freedom-house-president-as-new-voa-director-/7577060.html ]]

Forum

XS
SM
MD
LG