Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Januari 15, 2025 Local time: 04:50

Marco Rubio kuteuliwa kuwa Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani


Rais mteule wa Marekani Donald Trump, akiwa na Seneta wa Florida, Marco Rubio wakati wa kampeni kwenye ukumbi Dorton, Raleigh,,North Carolina.
Rais mteule wa Marekani Donald Trump, akiwa na Seneta wa Florida, Marco Rubio wakati wa kampeni kwenye ukumbi Dorton, Raleigh,,North Carolina.

Rais mteule wa Marekani Donald Trump, kwa haraka anajaza utawala wake mpya na maafisa wa Repablikan, ambao wamekuwa waaminifu zaidi kwake kisiasa katika miaka minne tangu aondoke madarakani.

Kulingana na vyanzo kadhaa vya habari vya Marekani, Trump analenga kuteua Seneta wa Florida Marco Rubio kuwa waziri wa mambo ya nje, na Gavana wa South Dakota Kristi Noem, kuwa waziri wa Usalama wa Ndani.

Wote Rubio na Noem walikuwa kwenye orodha ya watu ambao wangekuwa wagombea wenza, miezi kadhaa iliyopita. Ingawa Trump hatimaye alimteuwa Seneta wa Ohio, JD Vance, kuwa mgombea wake mwenza kwenye tiketi ta chama cha Repablikan, wote Rubio na Noem, waliendelea kuwa waaminifu kwake kisiasa hadi pale aliposhinda kwa urahisi uchaguzi wa wiki iliyopita dhidi ya Mdemokrat, makamu wa Rais Kamala Harris.

Trump pia amemlenga Michael Waltz ambaye ni mwakilishi wa Florida kama mshauri wa kitaifa wa usalama. Waltz mapema mwaka huu aliunga mkono pendekezo la mswada wa Repablikan la kubadili jina la uwanjwa wa ndege wa kimataifa wa Washington kuitwa Trump. Jumatatu Trump alimteuwa Thomas Homan kuwa mkuu wa kitaifa wa uhamiaji. Homan alikaimu nafasi hiyo kwenye muhula wa kwanza wa Trump.

Forum

XS
SM
MD
LG