Hayo yamesemwa na Jumapili na chaguo lake la mshauri wa kitaifa kwenye masuala ya usalama Michael Waltz. Waltz ambaye kwa sasa ni mbunge wa Florida ameambia televisheni ya Fox kipindi cha “Fox News Sunday” kwamba uamuzi wa utawala unaoondoka wa Rais Joe Biden wa kuruhusu Ukraine kutumia vilipuzi vya ardhini kama njia ya kuzuia wanajeshi wa Russia mashariki mwa Ukraine, ni sawa na hali iliokuwepo wakati wa Vita vya Kwanza vya Dunia.
Waltz amesema kuwa maamuzi yanahitajika kupitia mashauriano pana, ili kumaliza vita hivyo. Waziri wa Ulinzi wa Marekani Lloyd Austin wiki iliopita alisema kuwa Marekani inatuma vilipunzi vya ardhini huko Ukraine kutokana na kubadilika kwa hali ya mapigano upande wa mashariki ambako vita vimechacha.
Alisema kuwa vikosi vya Russia vina magari maalum ya kivita na kwa hivyo ni muhimu kwa Ukraine kuchukua hatua itakayodhibiti kasi yao. Waltz amesema kuwa Trump anayechukua madaraka Januari 20 ana wasi wasi kutokana na vita hivyo, lakini swali kuu ni jee, tunaweza kufanya nini ili kurejesha amani?
Forum