Kellog alikuwa mkuu wa utawala kwenye Baraza la Kitaifa la Usalama wakati wa mhula wake wa kwanza, na pia alikuwa mshauri wa kitaifa wa usalama wa aliyekuwa makamu rais wa Trump, Mike Pence. “Kwa pamoja tutarejesha amani kupitia nguvu wakati tukihakikisha usalama wa Marekani na dunia, “ Trump alisema kwenye taarifa iliomtangaza Kellog kuwa mjumbe.
Kellog hapo Julai alizungumza na VOA, akieleza mtazamo wake katika kumaliza vita vya Ukraine, maandishi yaliyo kwenye kitabu chake kwa jina, “An America First Approach to U.S National Security.” Wakati huo alipendekeza kwamba kwa kuwa Marekani ni sera rasmi, inahitaji kuzingatia sitisho la mapigano na mashauriano kuelekea kumalizwa kwa vita vya Ukraine.
Alisema kuwa Marekani ingeendelea kutoa silaha kwa Ukraine ili kuzuia Russia kushambulia tena hata baada ya sitisho la mapigano, kwa masharti kwamba Kyiv itakubali kuingia kwenye mazungumzo ya amani na Russia.
Forum