Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Januari 15, 2025 Local time: 05:12

Trump afanya uteuzi mwingine wa Mwanasheria Mkuu


Saa kadhaa baada ya mteule wake wa kwanza kujitoa, Rais mteule wa Marekani, Donald Trump, ametangaza chaguo lake jipya la mwanasheria mkuu kwa kumteua Pam Bondi.

Mwanasheria mkuu wa zamani wa Florida, Bondi, alikuwa ni miongoni mwa wanasheria wa timu ya mawakili wa Trump wakati wa kesi yake ya kwanza iliyokuwa nia ya kumuondoa madarakani.

Bondi amekuwa mwendesha mashitaka zaidi ya miaka 18, na alikuwa mwanamke wa kwanza kushikili wadhifa wa mwanasheria mkuu wa Florida.

Pia ni mshirika wa muda mrefu wa Trump, na mwenyekiti wa taasisi ya sera ya Marekani kwanza. Katika taarifa yake, Rais mteule Trump, alisifia kazi za Bondi, katika kufanikisha kusimamisha dawa za kulevya, na kupunguza vifo kwa watumiaji haramu wa dawa za Fentanyl.

Forum

XS
SM
MD
LG