Magufuli ameahidi kuendelea na mageuzi kwenye sekta ya madini ili kuhakikisha ukuaji wa uchumi wa asilimia 8 kila mwaka.
Amesema hayo wakati akianza muhula wake wa pili wa uongozi baada ya kushinda uchaguzi mkuu uliomalizika hivi karibuni.
Kwa mujibu wa shirika la habari la Reuters, kuchaguliwa tena kwa Waziri Mpango ni ishara ya imani aliyokuwa nayo Rais kwake ikizingatiwa kuwa taifa hilo lilishuhudia ukuaji wa uchumi wa asilimia 6.9 wakati akiwa waziri katika awamu ya kwanza uliomalizika.
Magufuli mwishoni mwa mwezi uliopita alitangazwa mshindi kwenye uchaguzi mkuu baada ya kushinda zaidi ya asilimia 84 ya kura licha ya upinzani kulalamika kuwa zoezi hilo liligubikwa na dosari.
Awali akilihutubia wabunge, Magufuli amesema kuwa nia yake ni kuona taifa likikuwa kiuchumi kwa asilimia 8 wakati sekta ya madini ikiendelea kufanyiwa mageuzi.