Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 23, 2024 Local time: 09:32

Marekani yasikitishwa na dosari za Uchaguzi Mkuu Tanzania


Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Mike Pompeo
Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Mike Pompeo

Serikali ya Marekani imeelezea wasiwasi wake mkubwa kuhusu ripoti za uhakika kwamba kulikuwa na kusambaa kwa dosari nyingi katika upigaji kura, kuingilia kati kwa huduma ya internet, ukamataji, na ghasia ambazo zimefanywa na majeshi ya usalama kote Tanzania Bara na Visiwani Zanzibar.

Hata hivyo taarifa iliyotolewa na serikali ya Marekani kupitia Wizara ya Mambo ya Nje imewapongeza Watanzania kwa kujaribu kutumia haki yao ya kupiga kura katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 28.

Wizara ya mambo ya nje hata hivyo imeeleza bayana kuwa itaendelea kuzisihi pande zote na kujizuia na mizozo yoyote inayoweza kutokea na hivyo kubuni njia za amani kupata suluhisho.

“Tunaisihi mamlaka nchini Tanzania kuchunguza shutuma za dosari na ghasia ambazo zinadaiwa kufanywa na majeshi ya usalama na kuhakikisha kwamba wahusika kisiasa wana fursa ya kupitia mfumo wa taasisi za kisheria ili matatizo hayo yapatiwe suluhisho kwa njia ya amani,” taarifa imeongezea.

Tunaitaka serikali ya Tanzania kuheshimu haki za binadamu na misingi ya uhuru kwa wote, ikiwemo uhuru wa kujieleza na haki ya kuandamana kwa amani, na kuhamasisha uhuru wa internet na kuhakikisha kuwa wale wote waliokamatwa wakati wa maandamano, wanapatiwa utaratibu wa ulinzi kama inavyostahili, taarifa imesema.

Marekani kwa kushirikiana na washirika wake, wanafikiria hatua za kuchukua ikiwa ni pamoja na kuweka masharti ya visa, kama inavyoona ni muafaka, kuwawajibisha wale ambao wamegundulika kuhusika na ukiukaji wa haki za binadamu na kuingilia kati utaratibu wa uchaguzi.

Taarifa ya wizara imesema watanzania kama walivyo watu wengine kwingineko, wanastahili uwazi na utawala wenye uwajibikaji, watendewe sawa kwa mujibu wa sheria, na wawe na uwezo wa kutumia haki zao bila ya khofu ya kulipiziwa kisasi.

“Ili kufanikisha malengo yetu yanayofana na kuendeleza uhusiano wa pamoja kunahitaji kuhakikisha kwamba wadau wote wanawakilishwa na wanaweza kwa ukamilifu kutekeleza majukumu yao katika Tanzania yenye demokrasia,” taarifa hiyo imesema.

XS
SM
MD
LG