Magufuli anaingia katika kipindi cha pili cha uongozi wake huku akitaka taifa hilo kuungana pamoja baada ya uchaguzi wakati upinzani nchini humo ukitangaza kutotambua ushindi wake.
Katika uwanja wa Jamhuri Jijini Dodoma, makao makuu mapya ya serikali kwa mara ya kwanza linafanyika tukio la kuapishwa Kiongozi mkuu wa Nchi.
Katika hotuba yake Rais Magufuli amesisitza umuhimu wa Watanzania kuungana pamoja baada ya uchaguzi kumalizika
Wakati huohuo Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan naye amekula kiapo kwa nafasi hiyo katika sherehe hizo. Tafrija hiyo imehudhuriwa na viongozi mbalimbali wa ndani na nje ya Nchi Wakiwemo Marais Yoweri Museveni wa Uganda, Emerson Mnangagwa wa Zimbabwe na Rais wa Comoro Azali Ossoumani.