Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 23, 2024 Local time: 07:08

Pecker wa gazeti la National Enquirer asema Trump alitaka kuficha fedheha iliyomkabili isiwafikie wapiga kura


Rais wa zamani wa Marekani Donald Trump alipokuwa mahakamani New York.
Rais wa zamani wa Marekani Donald Trump alipokuwa mahakamani New York.

Mchapishaji wa zamani wa gazeti la udaku David Pecker amerejea kizimbani kwa siku ya nne kama shahidi katika kesi ya uhalifu ya Donald Trump huko New York, Marekani.

Pecker ametakiwa kujibu maswali zaidi jinsi alivyofanya malipo ya dola 150,000 kwa haki za madai ya mhudumu kwa mahusiano ya kingono ya miezi kadhaa aliyokuwa nayo na rais wa baadaye.

Pecker siku ya Alhamisi aliliambia jopo la mahakama la watu 12 kuwa aliiamini habari ya Karen McDougal ya mahusiano na Trump licha ya kuwa alikuwa ameikanusha.

David Pecker
David Pecker

Pecker alitoa ushahidi kuwa Trump alitaka kuzuia taarifa hiyo yenye kumfedhehesha kuwafikia wapiga kura kabla ya kushiriki kwake katika kinyang’anyiro kijacho cha kuingia White House kilicho kuwa na mafanikio cha 2016. Trump hakusema kuwa alikuwa anataka habari hizo ziwafikie mke wake, Melania Trump, au mtoto wake wa kike, Ivanka Trump.

“ Je ilikuwa siyo kuhusu kile ambacho Melania angesema, au Ivanka?” Pecker alitoa ushahidi katika kesi ya kwanza ya aina yake ya rais wa zamani wa Marekani. “Kimsingi ilikuwa (kuhusu) athari gani itakuwepo katika kampeni na uchaguzi.”

Kuna wakati, Pecker alisema Trump alimuuliza, “Nifanye nini?”

Pecker alisema alimwambia Trump ni lazima “ainunue hiyo taarifa na kuiondoa hadharani,” lakini gazeti hilo la udaku lilifikia hatua ya kufanya hivyo kwa ajili yake. Pecker alisema gazeti hilo lilitarajiwa kulipwa, lakini hawakupata malipo yoyote.

Katika mahojiano yaliyofanywa na wakili wa utetezi wa Trump Emil Bove, Pecker alitoa ushahidi kuwa gazeti lake lililokuwa linauzwa katika duka la vyakula, The National Enquirer, aghlabu lilinunua habari mbalimbali zilizo kuwa za fedheha kuhusu watu mashuhuri kama vile Trump kuwalinda au kufikia makubaliano ya kufanya mahojiano nao kuhusu masuala hayo yenye utata kabla ya kuchapishwa.

Pecker alisema gazeti hilo la udaku aghlabu lilinunua taarifa na kuinyamazisha, utaratibu ambao ulikuja kujulikana kama “catch and kill.”

Pecker alisema kuwa kwa miaka kadhaa alikuwa mapema akimpa taarifa Trump zilizo na fedheha dhidi yake ambazo walizipata kuhusu yeye wakati alipokuwa ni mtu maarufu kwenye vilabu vya usiku na tajiri wa upangishaji majumba huko New York.

Pecker alitoa ushahidi mapema wiki hii kuwa alikuwa amefahamiana na Trump tangu mwaka 1980 na bado anamuona kuwa rafiki yake, hata pale ambapo anatoa ushahidi kama shahidi wa upande wa mashtaka.

FILE - David Pecker
FILE - David Pecker

Katika kumhoji Pecker Alhamisi, wakili wa Trump Bove alionekana kuwa anajaribu kuonyesha ununuaji wa habari ya McDougal ni biashara kama kawaida katika gazeti hilo, na hakuna mafungamano na tuhuma kadhaa zinazomkabili Trump mwenye umri wa miaka 77.

Trump, hivi sasa mgombea mtarajiwa wa urais kwa tiketi ya Republikan 2024 dhidi ya Rais Joe Biden katika uchaguzi wa Novemba, anatuhumiwa kughushi rekodi za biashara kuficha malipo aliyofanya ya dola 130,000 ya kumrubuni mcheza filamu za ngono Stormy Daniels ili kumfanya kutotoa taarifa za Trump kabla ya uchaguzi wa 2016 kuhusu madai ya ngono aliyofanya na Trump usiku mmoja muongo mmoja uliopita.

Trump amekanusha pia taarifa za mwanamke huyo na mashtaka yote 34 yanayomkabili katika kesi ya New York, moja ya mashtaka manne aliyofunguliwa ya aina yake dhidi ya rais wa 45 wa Marekani.

Trump amekanusha mashtaka yote 88 yanayomkabili, lakini kesi ya New York ndiyo inaelekea kuwa pekee itafanyika kabla ya uchaguzi wa Novemba 5. Utafiti wa maoni kitaifa unaonyesha kuwa baadhi ya wafuasi wa Trump wanaweza kubadilisha mawazo kuhusu kumpigia kura iwapo atapatikana na makosa.

Rais wa zamani Donald Trump
Rais wa zamani Donald Trump

Iwapo atakutwa na makosa, Trump anaweza kufungwa hadi miaka minne au kuwekewa masharti.

Pecker alisema katika mazungumzo yao mwaka 2016, Trump ,”alimuelezea McDougal kuwa “binti mzuri” na hivyo kuamini kuwa Trump “alikuwa anamjua mwanamke huyo.”

Mwaka mmoja baadaye, baada ya Trump kuwa Rais, Pecker alisema Trump alimuuliza “Karen anaendeleaje” wakati wakitembea katika viwanja vya White House. Pecker alisema alijibu kuwa anaendelea vizuri. “Yuko kimya,” alikumbuka alichomwambia Trump.

Forum

XS
SM
MD
LG