Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 23, 2024 Local time: 06:17

Hoja za ufunguzi zinatarajiwa kuanza katika kesi ya New York inayomkabili Donald Trump

Aliyekuwa Rais wa Marekani, Donald Trump akiwasili katika mahakama ya jinai ya Manhattan akiwa na timu yake ya wanasheria huko New York, NY siku ya Jumatatu, Aprili 15, 2024. Jabin Botsford.REUTERS.
Aliyekuwa Rais wa Marekani, Donald Trump akiwasili katika mahakama ya jinai ya Manhattan akiwa na timu yake ya wanasheria huko New York, NY siku ya Jumatatu, Aprili 15, 2024. Jabin Botsford.REUTERS.

Hoja za ufunguzi zinatarajiwa kuanza Jumatatu katika kesi ya New York inayomkabili Donald Trump, kesi ya kwanza ya jinai kuwahi kuwasilishwa dhidi ya rais wa zamani wa Marekani.

Hoja za ufunguzi zinatarajiwa kuanza Jumatatu katika kesi ya New York inayomkabili Donald Trump, kesi ya kwanza ya jinai kuwahi kuwasilishwa dhidi ya rais wa zamani wa Marekani.

Katika kuwasilisha kwa jopo la mahakama la watu 12 waendesha mashtaka wana uwezekano wa kudai kwamba Trump alipanga njama mwaka 2016, kabla ya kampeni yake ya White House iliyofanikiwa, kuficha malipo ya fedha kwa wanawake wawili ili kuficha madai yao ya mahusiano nae ya kimapenzi nje ya ndoa.

Waendesha mashtaka wanadai kwamba Trump alikuwa akitaka kuendelea kuficha taarifa za hatari kwake kuhusu maisha yake ya kibinafsi kutoka kwa wapiga kura, kabla tu ya upigaji kura miaka minane iliyopita.

Lakini mawakili wa Trump, kando na kukanusha maswala hayo, wana uwezekano wa kuliambia baraza la wazee wa mahakama kwamba rekodi za biashara za malipo ya Trump kwa Michael Cohen, zilidaiwa kumlipa kwa kazi yake ya kisheria na sio dola 130,000 kama fedha za kuzuia taarifa ambazo Cohen anadai kuwa alimlipa mwigizaji wa ponografia Stormy Daniels.

Forum

XS
SM
MD
LG