Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 10:10

Aliyejichoma moto New York nje ya mahakama ya kesi ya Trump afariki


Mwanamme mmoja aliyejichoma moto nje ya mahakama ambako kesi ya rais wa zamani wa Marekani, Donald Trump, inafanyika amefariki dunia polisi wamesema.

Idara ya polisi ya jiji la New York, imeiambia The Associated Press Jumamosi kwamba mtu huyo alitangazwa kuwa amekufa na wataalamu wa hospitali ya eneo hilo.

Mwanamme huyo alikuwa katika bustani ya Collect Pond, majira ya saa saba na nusu mchana wa Ijumaa, akitoa na kutupa vipeperushi vinavyounga mkono tetesi za njama kisha akajimwagia mafuta na kujichoma moto maafisa na mashahidi wamesema.

Idadi kubwa ya polisi walikuwepo karibu na eneo wakati hayo yanatokea. Baadhi yao na raia walikimbilia kumsaidia mtu huyo.

Kutokana na majeraha ya moto alilazwa hospitali akiwa katika hali mahutut. Mtu huyo inaelezwa alitokea Florida na kwenda New York siku chache zilizopita.

Forum

XS
SM
MD
LG