Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 16:15

Kesi nyingine ya Trump kuendelea Jumatatu


Donald Trump, anaelekea mahakamani Jumatatu, akiwa ni rais wa kwanza mstaafu wa Marekani kukabiliwa na mashtaka ya uhalifu na tishio la kufungwa jela iwapo atapatikana na hatia.

Mawakili wake, waendesha mashtaka na Jaji Juan Merchan wataanza kuchagua baraza la mahakama ya New York ili kusikiliza ushahidi wa madai ya shutuma kwa Trump, kumyamazisha na kuficha ukweli kwa kumpa pesa mchezaji wa filamu za ngono.

Trump, ambaye ni mgombea wa kiti cha urais wa chama cha Republican katika uchaguzi wa Novemba, atasikiliza mashitaka yake akiwa katika meza ya mshtakiwa wa kesi ambayo inaweza kusikilizwa kwa siku nne kwa wiki katika mwezi mmoja na nusu ujao.

Anaweza kuchukua msimamo wa kujitetea kama shahidi au la, kama yeye na mawakili wake watakavyoona kutokana na ushahidi wa waendesha mashtaka.

Forum

XS
SM
MD
LG