Hali ilikuwa ya kusisimua kwenye ukumbi wa Radio City Music ambapo Obama alimsifu Biden kwa kuwa na msimamo wenye kuzingatia kila mmoja, akisema kuwa ,” Huyo ndiyo rais tunayemtaka.”
Clinton kwa upande wake alisema kwamba miongoni mwa wanaowania kwenye uchaguzi wa mwaka huu, “Ni bora kubaki na anayefanya kazi.” Biden kwa upande wake alimtaja mpinzani wake Donald Trump moja kwa moja, akisema kwamba mipango ya mgombea huyo wa chama cha Repablikan imepitwa na wakati na wala haifai.
Aliyeongoza hafla hiyo Stephen Colbert, wakati akizungumza na viongozi hao watatu aliwaita “ mabingwa wa kuzungumza,” akitania kuwa wote walifika New York, siyo kwa ajili ya kufika mahakamani, akizungumzia matatizo mengi ya kisheria yanayomkabili Trump.
Hafla hiyo ya uchangishaji fedha ilikuwa ni uungaji mkono mkubwa wa chama cha Demokratic kwa Biden, wakati ukusanyaji maoni ukionyesha uungaji mkono mdogo.
Forum