Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 23, 2024 Local time: 15:34

Rais Biden aahidi kujenga tena daraja la Baltimore


Rais wa Marekani Joe Biden
Rais wa Marekani Joe Biden

Rais wa Marekani Joe Biden Jumanne ameeleza kubomoka kwa daraja la Baltimore ni “ajali mbaya,” na kuahidi kurejesha huduma za bandari kuu ya East Coast kwa haraka iwezekanavyo baada ya meli ya mizigo kugonga nguzo ya daraja hilo.

Biden pia alisema daraja la Francis Scott Key Bridge litajengwa tena kwa haraka iwezekanavyo lakini alikiri “itachukua muda kidogo.” Amesema atapeleka “fedha zote za serikali kuu wanazohitaji “ kukabiliana na ajali hiyo.

Wakati huo huo Kikosi cha uokoaji na utafutaji kinaendelea na zoezi la kuwatafuta watu 20 waliotoweka baada ya daraja kuu kubomoka katika mji wa Baltimore, Maryland ulioko kusini mwa Marekani⁣

Video iliyochukuliwa kwa simu ya mkononi ilionyesha vipande kadhaa vya Daraja la Scott Key likiporomoka ndani ya maji ya Mto Patapsco baada ya meli iliyobeba mizigo yenye bendera ya Singapore inayoitwa Dali kugonga nguzo inayoshikilia daraja majira ya saa kumi na moja alfajiri (05:30 UTC) Jumanne. ⁣

Mamlaka zinasema magari kadhaa yalikuwa juu ya daraja wakati ajali hiyo ilipotokea.⁣

Maafisa wa huduma za dharura wa Baltimore kikosi cha watafutaji na waokoaji kinaendelea kuwatafuta watu wasiopungua 20 ambao wanasadikiwa kuwa ndani ya maji.

Daraja la Baltimore
Daraja la Baltimore



Magari kadhaa yalianguka kwenye maji baridi na waokoaji walikuwa wakitafuta zaidi ya watu saba.⁣

Wanasema vyombo vyao vimebaini kuna magari yaliyotumbukia mtoni. ⁣
Inaonekana Meli hiyo iligonga nguzo moja ya daraja Fransis scott key Bridge ambapo lilivunjika vipande, kulingana na picha zilibandikwa katika mtandao wa X. ⁣

Meli hiyo ilisababisha moto ulitoa moshi mweusi ulopaa hewani. ⁣
Meli hiyo inayosafiri na bendera ya Singapore na jina la Dali ilikuwa imeondoka bandarini dakika 25 zilizopita ikielekea Singapore. ⁣

Synergy Marine Corp, Wasimamizi wa meli ya Dali, wametoa taarifa wakisema meli hiyo iligonga moja ya nguzo za daraja hilo na kuwa mabaharia wake wote, wakiwemo nahodha wa meli hiyo wamesalimika na hakuna ripoti zozote za majeruhi.



Daraja hilo lenye urefu wa kilomita 2.5 lenye umri wa miaka 47 ni kiungo kikuu katika njia kuu zinazounganisha majimbo zinazo zunguka mji wa Baltimore, moja ya bandari kadhaa kubwa kabisa za Marekani.⁣

Ilipewa jina la Francis Scott Key, mwandishi wa “The Star Spangled Banner,” shairi ambalo baadae lilitengenezwa kuwa muziki na hatimaye kuwa ni nyimbo ya taifa ya Marekani.⁣

Key alihamasishwa kuandika shairi baada ya kushuhudia mashambulizi ya bomu yaliyofanywa na Uingereza katika ngome kuu ya jeshi la Marekani huko Baltimore mwaka 1814.

Baadhi ya taarifa hii inatokana na mashirika ya habari ya AP, AFP, Reuters

Forum

XS
SM
MD
LG