Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 23:54

Daraja kubwa laporomoka baada ya kugongwwa na meli ya mizigo Baltimore Md Marekani

Daraja la la Francis Scott Key likiwa limeporomoka, baada ya kugongwa nguzo na meli ya makontena ya Dali, ikipelekea magari mengi na watu kutumbukia kwenye mto.Kamishna wa Polisi wa Baltimore Richard Worley alisema hakuna dalili za ugaidi. Baltimore, Maryland, Machi 26, 2024.

Timu za kutafuta na kuokoa zinawatafuta karibu watu 20 ambao hawajulikani walipoa baada ya daraja kubwa kuporomoka katika mji wa Baltimore, Maryland Marekani.

Video ya simu ilionyesha sehemu kadhaa za daraja hilo la Francis Scott Key likianguka kwenye Mto Patapsco baada ya meli ya kontena yenye bendera ya Singapore inayoitwa Dali kugonga nguzo ya Daraja hilo Jumanne alfajiri.

Maafisa wa usalama waasema magari kadhaa yalikuwa kwenye daraja wakati ajali hiyo ilipotokea.

Maafisa wa dharura wa Baltimore wanasema wafanyakazi wa utafutaji na uokoaji wanatafuta takriban watu 20 wanaoaminika kuwa ndani ya maji.

Wasimamizi wa meli ya Dali, Synergy Marine Corp, walitoa taarifa wakisema kuwa meli hiyo iligonga nguzo moja ya daraja hilo na kwamba wafanyakazi wake wote wakiwemo manahodha wawili waliokuwemo wamepatikana na hakuna taarifa zozote za majeruhi

Forum

XS
SM
MD
LG