Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Novemba 05, 2024 Local time: 13:39

Waziri Blinken akutana na Waziri wa Ulinzi wa Israel

Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken (wa kwanza kushoto) akiwasili Israel.
Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken (wa kwanza kushoto) akiwasili Israel.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken akutana na Waziri wa Ulinzi wa Israel Yoav Gallant Jumatatu katika Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani mjini Washington.

Blinken alikutana na Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu na maafisa wengine wa Israel Ijumaa iliyopita mjini Tel Aviv ili kushinikiza sitisho la vita kwa muda wa wiki sita kati ya Israel na Hamas.

Pia aliili kubadilishana na kuachiliwa kwa mateka waliokamatwa katika shambulio la kigaidi la Oktoba 7.

Blinken alisisitiza nia ya utawala wa Biden dhidi ya mipango ya Israel ya kuanzisha mashambulizi makali kwenye mji wa kusini mwa Gaza wa Rafah, ambapo mamilioni ya wakimbizi wa Kipalestina wanajihifadhi kwenye mahema ya muda.

Watoto wa Kipalestina wakisimama katikati ya kifusi cha jengo huko katika kambi ya wakimbizi wa Kipalestina ya Maghazi lililo haribiwa vibaya sana na shambulizi la Israel katika mgogoro unaoendelea kati ya Israel na kikundi cha wanamgambo wa Palestina, Hamas.

Wakimbizi hao walisukumwa huko zaidi kutoka kwa wanajeshi wa Israel, ambao waliwaambia waondoke makwao kaskazini mwa Gaza huku wanajeshi wa Israel wakisonga mbele huko katika hatua za awali za vita.

Blinken alisema shambulio hilo litahatarisha raia wengi zaidi wa Palestina, pamoja na kuitenga zaidi Israel duniani kote.

Forum

XS
SM
MD
LG