Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 23:43

Jeshi la Marekani limeshambulia vituo vitatu vya kuhifadhi silaha huko Yemen


Wafuasi wa ki-Houthi wakipinga mashambulizi ya anga ya Marekani huko Yemen pamoja na mashambulizi ya Israel huko Gaza. Yemen, March 8, 2024.
Wafuasi wa ki-Houthi wakipinga mashambulizi ya anga ya Marekani huko Yemen pamoja na mashambulizi ya Israel huko Gaza. Yemen, March 8, 2024.

Vikosi vya Marekani vilifanya mashambulizi ya kujilinda dhidi ya vituo vya kuhifadhi silaha vya chini ya ardhi vya wa-Houthi

Jeshi la Marekani limesema Ijumaa kuwa limeshambulia vituo vitatu vya kuhifadhia silaha vya chini ya ardhi vinavyotumiwa na waasi wa ki-Houthi nchini Yemen, wakati waasi wanaoungwa mkono na Iran wakiendelea kufanya mashambulizi kwenye meli katika bahari ya Sham.

Vikosi vya Marekani vilifanya mashambulizi ya kujilinda dhidi ya vituo vitatu vya kuhifadhi silaha vya chini ya ardhi vya wa-Houthi katika maeneo yanayodhibitiwa na wa-Houthi wanaoungwa mkono na Iran huko Yemen, Central Command (CENTCOM) imesema katika taarifa.

Imesema vikosi vya Marekani pia vimefanikiwa kuyashambulia na kuharibu ndege nne zisizo na rubani katika maeneo yanayodhibitiwa na Wa-houthi nchini Yemen siku ya Ijumaa, wakati pia yakisajili makombora manne ya masafa marefu yaliyorushwa na waasi wa ki-Houthi kuelekea Bahari ya Shamu.

“Hakuna majeruhi au uharibifu ulioripotiwa na Marekani, muungano au meli za kibiashara”, CENTCOM ilisema. Wa-houthi walianza kushambulia meli katika Ghuba ya Aden na Bahari ya Shamk mwezi Novemba, kampeni ambayo wanasema inalenga kuashiria mshikamano na raia wa-Palestina huko Gaza.

Wameapa kuzilenga meli za Israel, Uingereza na Marekani, pamoja na meli zinazoelekea katika bandari za Israel, na kuvuruga usafiri kupitia njia muhimu ya kibiashara katika pwani ya Yemen.

Forum

XS
SM
MD
LG