Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 09:53

Kampeni ya Biden yafuatilia tukio moja la rekodi ya uchangishaji fedha wa Trump


Rais wa Marekani Joe Biden (D), kulia, na Rais wa zamani Donald Trump (R).
Rais wa Marekani Joe Biden (D), kulia, na Rais wa zamani Donald Trump (R).

Katika mahojiano na VOA, kampeni ya Rais Joe Biden ya kutaka kuchaguliwa tena haikutilia maanani tukio moja la rekodi ya uchangishaji fedha lililofanyika Jumamosi na kampeni ya Donald Trump.

Wachambuzi wameelezea, hata hivyo, kwamba fedha peke yake haziwezi kumpa uhakika mgombea kurejea White House.

Akiweka rekodi mpya katika tukio pekee la uchangishaji fedha, kampeni ya Trump ilichangisha takriban dola milioni 50.5 siku ya Jumamosi wakati wa halfa kwa ajili ya wafadhili matajiri huko Palm Beach, Florida. Alipowasili katika eneo la tukio, mgombea mtarajiwa wa Republican, Donald Trump, alielezea imani yake kwa mafanikio ya hafla hiyo.

Donald Trump, Mgombea Urais Mtarajiwa wa Republican anaeleza: “Watu, walitaka kuchangia kwasababu ya kuifanya America kuwa nzuri tena. Watu matajiri wanataka, watu maskini wanataka, kila mtu anataka mabadiliko. Nchi kwa kweli haifanyi vizuri. Tumekuwa kituo tunachekwa kila mahali duniani na haraka sana tutaleta mabadiliko.”

Rais wa zamani wa Marekani Donald Trump.
Rais wa zamani wa Marekani Donald Trump.

Kampeni ya Rais Mdemocrat Joe Biden, ambaye anawania kuchaguliwa tena, pia imetoa kiwango cha uchangishaji fedha wa karibuni mwishoni mwa wiki.

Msemaji mwandamizi Kevin Munoz ameiambia VOA Jumapili kwamba wamarekani milioni 1.6 wametoa michango mikubwa na kuelezea jinsi kampeni itakavyotumia dola milioni 192 fedha taslimu ambazo wanazo mkononi.

Kevin Muñoz, Kampeni ya Biden-Harris anaeleza: “Zaidi ofisi 100 kote katika majimbo yenye ushindani mkali. Mamia ya wafanyakazi wako kote katika majimbo haya yenye ushindani mkali, historia ya dola milioni 30 zimelipiwa kampeni iliyolenga API, wapiga kura Walatino na Wamarekani Wuesi wakizungumza na wapiga kura hawa mapema na mara nyingi wakielezea maamuzi katika uchaguzi huu.”

Rais wa Marekani Joe Biden akiwa White house Desemba 11, 2023. Picha na Reuters
Rais wa Marekani Joe Biden akiwa White house Desemba 11, 2023. Picha na Reuters

Muñoz pia alipuuza mafanikio ya karibuni ya uchangishaji fedha uliofanywa na kampeni ya Trump.

Kevin Muñoz, Kampeni ya Biden-Harris: “Wafadhili wa juu wa kampeni ya Joe Biden ni wauguzu na waalimu. Sisi tuna nguvu ya wafanyakazi na kwamba ni kinyume sana na kampeni ya Donald Trump. Hili ndiyo linaloendelea ili kushinda uchaguzi.”

Lakini fedha peke yake hazitasaidia kurejea White House kwa Biend au Trump, wachambuzi wameelezea.

Mark Hansen, Profesa Chuo Kikuu cha Chicago: “Tatizo kubwa ni kwamba Rais Biden anakabiliwa hivi sasa na mipasuko ndani ya chama chake na kujiondoa ni kwa kweli ni kuwafikia watu ambao ni huru hawana chama. Watu ambao pengne hawajali kuhusu Warepublican.”

Steffen Schmidt, Profesa Chuo Kikuu cha Iowa anasema: “Trump ana msingi thabiti. Ana shauku kubwa, watu wenye nia ya dhati, lakini sina uhakika kuwa namba zinaonyesha kuwa msingi wake umeongezeka sana.”

Kampeni ya Trump haijajibu ombi la VOA kufanya mahojiano, lakini kwenye tovuti yake, limetangaza kuwa mkutano wa Trump utakuwa April 13 huko Pennyslvania.

Ajenda ya kampeni ya Biden itakuwa na shughuli nyingi katika wiki hii.

Rais wa Marekani Joe Biden na Makamu wa Rais Kamala Harris.
Rais wa Marekani Joe Biden na Makamu wa Rais Kamala Harris.

Kevin Muñoz, Kampeni ya Biden-Harris anaeleza: “Angalia, anaelekea Madison, Wisconsin kesho kuzungumza kuhusu mikopo ya wanafunzi. Pia ana tukio jingine la uchangishaji fedha. Atazungumza na wapiga kura ambao watafanya maamuzi kuhusu uchaguzi kila siku kati ya sasa na Novemba.”

Uchangishaji fedha utafanyika Chicago wiki hii, Munoz amesema bila ya kutoa maelezo zaidi. Rais pia atahitaji kushughulikia masuala ya ndani na kimataifa katika wiki nzima. Ikiwa ni pamoja na ziara ya Waziri Mkuu wa Japana, Fumio Kishida.

Forum

XS
SM
MD
LG