Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 23, 2024 Local time: 01:35

Mahakama ya Juu kusikiliza hoja ya Rais wa zamani Trump kuhusu kupewa kinga


Rais wa zamani wa Marekani Donald Trump akizungumza na waandishi wa habari mahakamaniNew York, Apriil 22, 2024.
Rais wa zamani wa Marekani Donald Trump akizungumza na waandishi wa habari mahakamaniNew York, Apriil 22, 2024.

Mahakama ya Juu ya Marekani imepanga kipindi maalum kusikiliza hoja kama Rais wa zamani Donald Trump anaweza kushitakiwa kwa juhudi zake kutaka kuvuruga Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2020 ambapo alishindwa  na Rais Joe Biden.

Kesi inayotakiwa kujadiliwa Alhamisi ni kuhusu majaribio ya Trump kutaka mashtaka dhidi yake yatupiliwe mbali. Mahakama za chini zimegundua kuwa hawezi kudai kwa hatua ambazo waendesha mashataka wanasema zilitaka kuingilia matokeo ya uchaguzi kinyume cha sheria.

Trump ameshitakiwa katika mahakama ya serikali mjini Washington, kwa kula njama ya kutaka kutengua uchaguzi wa mwaka 2020 moja wapo ya kesi nne za uhalifu anazokabiliwa nazo . kesi ilianza mjini New York kuhusu malipo ya pesa yanayojulikana kama hush- money kwa nyota wa filamu za ngono ili kuficha tuhuma za ngono.

Mahakama ya juu inakwenda mbio kuliko kawaida katika kushughulikia kesi hii ingawa siyo haraka kama mwendesha mashtaka maalumu Jack Smith alivyotaka, ikizusha maswali kuhusu kama kutakuwa na muda kufanya kesi kabla ya uchaguzi mkuu wa Novemba endapo majaji watakubaliana na mahakama za chini kwamba Trump anaweza kushitakiwa.

Jack Smith
Jack Smith

Baadhi ya taarifa katika habari hii zinatokana na shirika la habari la AP.

Forum

XS
SM
MD
LG