Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Januari 22, 2025 Local time: 07:11

White House inatathmini njia za kutoa hadhi ya muda na vibali kwa wahamiaji wanaoishi kinyume cha sheria


Rais Joe Biden akizungumza katika Prince William Forest Park kuadhimisha siku ya mazingira Duniani , Jumatatu, Aprili 22, 2024, huko Triangle, Va.
Rais Joe Biden akizungumza katika Prince William Forest Park kuadhimisha siku ya mazingira Duniani , Jumatatu, Aprili 22, 2024, huko Triangle, Va.

White House inatathmini njia za kutoa hadhi ya muda ya kisheria na vibali vya kufanya kazi kwa wahamiaji nchini Marekani wanaoishi kinyume cha sheria.

White House inatathmini njia za kutoa hadhi ya muda ya kisheria na vibali vya kufanya kazi kwa wahamiaji nchini Marekani wanaoishi kinyume cha sheria ambao wameoa na kuolewa na raia wa Marekani, vyanzo vitatu vinavyofahamu suala hilo vilisema Jumatatu, hatua ambayo inaweza kuwapa nguvu baadhi ya Wademokrat kabla ya uchaguzi wa Novemba.

Wabunge wademokrat na mashirika ya utetezi yamemshinikiza Rais Joe Biden kuchukua hatua za kuwalinda wahamiaji nchini Marekani kinyume cha sheria huku Biden akizingatia wakati huo huo hatua za kiutendaji kupunguza kuvuka mipaka kinyume cha sheria.

Uhamiaji umeibuka jambo la wasiwasi wa juu kwa wapiga kura, haswa miongoni mwa Warepublican kabla ya uchaguzi wa Novemba 5 ukimshindanisha Biden, Mdemocrat, na mtangulizi wake wa Republican, Donald Trump. Trump amesema sera za Biden zenye vizuizi kidogo zimesababisha kuongezeka kwa uhamiaji haramu.

White House katika miezi ya hivi karibuni imezingatia uwezekano wa hatua za kiutendaji kuzuia wahamiaji katika mpaka wa Marekani na Mexico ikiwa vivuko vitafikia kizingiti fulani, na hivyo kuzua ukosoaji kutoka kwa baadhi ya Wademokrat na mawakili.

Forum

XS
SM
MD
LG