Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Novemba 23, 2024 Local time: 15:05

Mdahalo wa Vance na Walz wajadili haki ya Israel kujihami dhidi ya Iran


Gavana Walz na Seneta Vance wakisalimiana kabla ya kuanza kwa mdahalo wa wagombea makamu rais, Jumanne usiku, 01.10.2024, New York, Marekani.
Gavana Walz na Seneta Vance wakisalimiana kabla ya kuanza kwa mdahalo wa wagombea makamu rais, Jumanne usiku, 01.10.2024, New York, Marekani.

Seneta wa Marekani JD Vance, mgombea mwenza wa Donald Trump wa chama cha Republikan, alishindana na Gavana wa Minnesota Tim Walz, ambaye ndiye mgombea mwenza wa Kamala Harris wa chama cha Demokratik katika mdahalo wa televisheni ya kitaifa siku ya Jumanne.

Walz (kushoto) na Vance wakiwa New York
Walz (kushoto) na Vance wakiwa New York

Mdahalo huo huenda ukawa wa mwisho wa kampeni za urais 2024, na uwezekano wa kuupa uzito wa ziada kabla ya uchaguzi wa Novemba 5.

Swali la kwanza la mdahalo lilihusiana na mzozo unaoendelea katika Mashariki ya Kati, wote wawili waliulizwa kama wangeunga mkono mashambulizi ya awali ya Israel dhidi ya Iran ili kuvuruga maendeleo na mipango ya nyuklia ya nchi hiyo.

Hata hivyo hakuna aliyekuwa na shauku ya kujibu.

Walz alionekana kuwa na wasiwasi alikwepa swali hilo, akikosoa rekodi ya Trump katika utawala wake wa miaka minne madarakani.

"Cha msingi hapa ni kwamba uongozi thabiti utakuwa muhimu," Walz alisema.

"Ni wazi, na ulimwengu uliliona hilo kwenye mdahalo wiki chache zilizopita, Donald Trump mwenye umri wa karibu miaka 80 akizungumzia ukubwa wa umati sio tunachohitaji kwa wakati huu."

Rais wa zamani wa Marekani Donald Trump
Rais wa zamani wa Marekani Donald Trump

Vance kwa upande wake alionekana kumshutumu Walz kwa kutojibu swali moja kwa moja, lakini akajiingiza katika maelezo ya wasifu wake.

"Mama yangu alihitaji msaada wa chakula kwa muda wa maisha yake," alisema Vance, ambaye aliishi katika familia ya wafanyakazi wa Ohio.

Vance hatimaye alirejea kujibu swali hilo, akisema utawala wa pili wa Trump ungeunga mkono uamuzi wa Israel kuhusu suala hilo. Lakini si kabla ya kutoa utetezi wa muda mrefu wa sera ya mambo ya nje ya Trump, akionyesha muda wake wa uongozi kama wa amani isiyo ya kawaida.

Katika mazungumzo ya ufunguzi, angalau, wagombea hawakuwa na hamu ya kuzama katika maelezo ya sera kuliko walivyokuwa katika kutetea urithi wa Trump na kujitambulisha kwa Wamarekani.

Forum

XS
SM
MD
LG