Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 23, 2024 Local time: 14:59

Marekani: Kanda ya video ikionyesha afisa wa polisi akimuua aliyeshambulia watu kwa bunduki yatolewa kwa umma


FILE - Watu wakitoka katika eneo la maduka huku mikono yao ikiwa juu baada ya shambulizi la bunduki la Mei 6, 2023 huko Allen, Texas.
FILE - Watu wakitoka katika eneo la maduka huku mikono yao ikiwa juu baada ya shambulizi la bunduki la Mei 6, 2023 huko Allen, Texas.

Polisi wametoa kanda  ya video Jumatano ya afisa wa polisi akimuua mtu mwenye bunduki ambaye ni mwenye kuunga mkono msimamo mkali wa kundi la Wanazi, na kumaliza kwa haraka shambulizi la watu wengi ambalo liliua watu wanane na wengine saba kujeruhiwa katika eneo la maduka huko Dallas.

Maelezo ya video ya dakika tano na nusu iliyohaririwa yanaonyesha harakati za mwisho za Mauricio Garcia, 33, baada ya kumimina risasi kadhaa kutoka katika bunduki akina ya AR-15 katika maduka ya Allen Premium Mei 6.

Wale waliouliwa ni pamoja na wanafamilia watatu Wamarekani wenye asili ya Korea akiwemo mtoto wa miaka mitatu, mabinti wawili wadogo, mlinzi na mhandisi kutoka India.

Polisi bado hawajatoa taarifa kuhusu kile kilichompa motisha mtu huyo kufanya shambulizi.

Shambulizi hilo la bunduki limekuja katika mwaka mmoja ulioshuhudia wimbi la mauaji ya watu wengi ambalo halijawahi kutokea.

FILE - Watu wakusanyika upande wa pili wa barabara kutoka eneo la maduka baada shambulizi la bunduki Mei 6, 2023, in Allen, Texas.
FILE - Watu wakusanyika upande wa pili wa barabara kutoka eneo la maduka baada shambulizi la bunduki Mei 6, 2023, in Allen, Texas.

Picha hizo za video kutoka katika kamera aliyoivaa afisa wa polisi wa Allen inaanza kwa kuonyesha afisa huyo akiwaambia watoto wawili nje ya eneo hilo la maduka wavae mikanda yao na wawe watulivu.

Muda mfupi baadaye, sauti za mfululizo za milio ya risasi zinasikika kutoka katika eneo la maduka hayo.

Watoto wakiwa na mwanamke mmoja wanakimbia wakati afisa wa polisi akituma ujumbe kwa njia ya radio, anachukua silaha yake kutoka katika gari lake na kukimbilia kwenye milio ya risasi inaposikika, picha za video za kamera aliyoivaa zinaonyesha.

Wakati akikimbia, afisa huyo anawapigia watu kelele kuwaambia watu wasogee na waondoke katika eneo hilo. Wakati mmoja, anamwambia yule anayepokea taarifa zake, “Naamini tumempata muuaji huyu wa watu wengi” na kumpigia kelele mtu huyo mwenye silaha adondoshe chini silaha yake. “ Ninawapita watu waliojeruhiwa,” aliongeza kusema.

Afisa huyo anaendelea kukimbia akipita nje ya maduka kadhaa huku milio ya risasi ikiendelea kusikika. Katika dakika ya nne hivi kwenye video hiyo, afisa huyo anafyatua risasi na kutumia takriban risasi nusu darzeni.

Muda mfupi baadaye, afisa huyo anapiga kelele: “Dondosha bunduki hiyo!” na kisha anaripoti: “Nimeweza kumdondosha chini!”

Afisa mwingine baadaye anathibisha kuwa mtu aliyekuwa ana bunduki amefariki.

Picha za video hizo zinamalizika zikionyesha maafisa hao wawili wakiwa wamesimama mbele ya mwili wa mtu aliyekuwa na bunduki, ambayo haionekani vizuri.

Picha za video hiyo zilitolewa siku moja baada ya jopo la washauri wa mahakama lilipomkuta afisa huyo hana hatia, likisema kuwa “matumizi ya nguvu za ziada yalihalalishwa chini ya sheria za Texas,” kwa mujibu wa taarifa ya polisi.

Katika taarifa hiyo, Mkuu wa Polisi wa Allen Brian Harvey alimpongeza afisa huyo wa polisi.

Chanzo cha habari hii ni shirika la habari la AP.

Forum

XS
SM
MD
LG