Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Januari 22, 2025 Local time: 22:13

Marekani: Watu watano wauawa katika shambulizi la bunduki mjini Louisville


Shambulizi la bunduki huko mjini Louisville, Kentucky, Marekani
Shambulizi la bunduki huko mjini Louisville, Kentucky, Marekani

Watu watano wameuawa na wengine sita wamelazwa hospitali katika shambulizi la bunduki kwenye jengo la benki Jumatatu asubuhi mjini Louisville, polisi walisema.

Mshukiwa katika shambulizi hilo pia amefariki, Naibu Mkuu wa Polisi huko Louisville Paul Humphrey ameuambia mkutano wa waandishi wa habari.

Walioshuhudia tukio hilo ambao waliondoka katika jengo hilo wamekiambia kituo cha televisheni cha Louisville cha WHAS walisikia mlio wa bunduki ndani ya jengo hilo.

Magari kadhaa ya polisi yalionekana katika picha za video za televisheni. Waandishi wa WHAS walisema wamewaona watu wakichukuliwa na magari ya kubeba wagonjwa kutoka katika eneo la tukio.

Katika ujumbe wa Twitter, Gavana wa Kentucky Andy Beshear alisema anaelekea katika eneo la tukio hilo.

“Naomba muziombee familia zote zilizoathiriwa na tukio hili na kwa mji wa Louisville,” Beshear alisema.

Idara ya Upelelezi (FBI) imesema mawakala wake walikuwa walikabiliana na shambulizi hilo.

Chanzo cha habari hii ni shirika la habari la AP

XS
SM
MD
LG