Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 23, 2024 Local time: 20:30

Bendera kupeperushwa Ikulu ya Marekani kuomboleza vifo vya mauaji ya Nashville


Wanafunzi wakiwa katika maombi ya maomboleza ya shambulizi la wengi katika shule huko Nashville.
Wanafunzi wakiwa katika maombi ya maomboleza ya shambulizi la wengi katika shule huko Nashville.

Bendera kwenye ikulu ya Marekani pamoja na majengo ya serikali, zitapeperushwa nusu mlingoti hadi machi 31  jioni kufuatia vifo vya wanafunzi watatu na watu wazima watatu kwenye shule ya Nashville  katika jimbo la Tennessee, kutokana na shambulizi la risasi Jumatatu, Machi 27.

Katika taarifa yake Rais wa Marekani Joe Biden amesema amechukua hatua hiyo kama heshima kwa walioathiriwa na vitendo visivyokuwa na maana vya vurugu vilivyotokea Jumatatu huko Nashville.

Mshambuliaji mwenye silaha nzito Audrey Hale mwenye umri wa miaka 28 , mwanafunzi wa zamani wa shule ya Covenant , aliyetambuliwa kama mtu aliyebadili jinsia aliuawa wakati akipambana na maafisa wa polisi watano wakati wa shambulizi hilo lililotokea kwenye ghorofa ya pili katika shule ya Presbyterian ambayo inahusiana na kanisa , maafisa wamesema.

Biden aliwaambia waandishi wa habari baada ya shambulizi la risasi , ilikuwa ndoto mbaya katika familia akirejea wito wake kwa bunge kupitisha marufuku ya matumizi ya silaha za mashambulizi.

Rais wa Marekani wa Marekani: “Nataka kuzungumza kwa ufupi kuhusu ufyatuaji risasi kwenye shule huko Nashville Tennessee. Mnafahamu kwamba Ben na mimi tumekuwa tukishinikiza hili kwa muda mrefu . Ni jambo la kuhuzunisha. Tumekuwa tukikusanya data kuhusu kilichotokea, na kwa nini. Kuna watu wengi ambao hawatafika wanapokwenda, wakiwemo watoto. Familia nyingi zinahofia hilo.”

Wanafunzi waliouwawa ni Evelyn Dieckhaus, Hallie Scruggs na Wiiliam Kinney, wote walikuwa na umri wa miaka 9.

XS
SM
MD
LG