Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Novemba 23, 2024 Local time: 11:32

Wanamgambo wanaoshukiwa wa ADF wameuwa takriban watu 17 mashariki mwa DRC


Muonekano wa nyumba iliyoteketea wakati wa mashambulizi ya watu wanaoshukiwa kuwa wanachama wa kundi la waasi la Allied Democratic Forces (ADF), katika kijiji cha Mukondi, Kusini mwa Beni, mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Machi 10, 2023.REUTERS
Muonekano wa nyumba iliyoteketea wakati wa mashambulizi ya watu wanaoshukiwa kuwa wanachama wa kundi la waasi la Allied Democratic Forces (ADF), katika kijiji cha Mukondi, Kusini mwa Beni, mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Machi 10, 2023.REUTERS

Wanamgambo wanaoshukiwa kuwa wa ADF siku ya Jumapili waliwauwa takriban watu 17 mashariki mwa DRC, maafisa wa eneo hilo walisema, siku chache tu baada ya kundi hilo lenye mafungamano na kundi la kigaidi la Kiislamu kufanya mauaji mengine katika eneo hilo lenye machafuko.

Kundi hilo la Allied Democratic Forces (ADF), ambalo kundi la Islamic State linadai kuwa ni mshirika wake wa kati kati mwa Afrika, ni mojawapo ya wanamgambo wabaya zaidi mashariki mwa Congo, wanaotuhumiwa kuwaua maelfu ya raia.

Shambulizi la hivi karibuni lilitokea asubuhi ya Jumapili huko Kirindera katika jimbo la Kivu Kaskazini katika eneo la Beni, kulingana na chifu wa kijiji Katembo Kahongya.

"Tuna watu 17 waliofariki na wanne wamejeruhiwa," aliiambia AFP, akiongeza kuwa wanamgambo hao pia wamechoma majengo.

Walitumia silaha za mapanga na moto kuwaua watu," Kahongya alisema.

Aliyekuwa Gavana wa Kivu Kaskazini Carly Nzanzu Kasivita pia alitweet kwamba watu wanaoshukiwa kuwa wapiganaji wa ADF walikuwa wamewaua watu 19 katika kijiji hicho, akibainisha kuwa idadi hiyo ilikuwa ya muda tu.

Mkazi wa Kirindera, Mukondano Kambale alisema wanamgambo hao waliwaua watu katika hoteli na zahanati ya afya kabla ya kufukuzwa.

XS
SM
MD
LG