Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Desemba 24, 2024 Local time: 02:48

Mahakama Chad yawahukumu zaidi ya waasi 400 kifungo cha maisha jela


Watu wanaandamana huko Moundou, Chad, Oktoba 20, 2022. REUTERS
Watu wanaandamana huko Moundou, Chad, Oktoba 20, 2022. REUTERS

Mahakama nchini Chad iliwahukumu zaidi ya waasi 400 kifungo cha maisha jela siku ya Jumanne kuhusiana na kifo cha rais wa zamani Idriss Deby, ambaye aliuawa akiwa mstari wa mbele wa vita dhidi ya kundi lao mwaka 2021, wakili wao alisema.

Kesi ya wanachama 465 wa kundi la waasi la Front for Change and Concord in Chad (FACT) lenye makao yake nchini Libya ilianza Februari 13 katika mji mkuu wa Chad, N'Djamena.

Chumba cha kusikiliza kesi ya uhalifu cha mahakama ya rufaa ya N'Djamena Jumanne kiliwakuta washtakiwa 441 na hatia ya vitendo vya ugaidi, kudhoofisha usalama wa taifa na kuhatarisha maisha ya mkuu wa nchi miongoni mwa mashtaka mengine. Kiongozi wa FACT Mahamat Mahadi alikuwa miongoni mwao.

Walihukumiwa kifungo cha maisha jela na watalazimika kulipa fidia kwa serikali, wakili wao Francis Djokoulde alisema.

Wengine waliachiliwa huru kwa sababu ya ukosefu wa ushahidi, alisema, akiongeza kuwa timu yake itakata rufaa katika Mahakama ya Juu.

Msemaji wa FACT Adoum Chouwimi alisema kesi hiyo ilikuwa na dosari na kuita uamuzi huo kuwa uongo mtupu.

Mapambano ambayo tumelazimika kutumia silaha yataendelea, Chouwimi alisema.

Deby, mwenye umri wa miaka 68 alipigwa risasi alipokuwa akiwatembelea wanajeshi waliokuwa kwenye mstari wa mbele dhidi ya waasi wa FACT ambao walikuwa wamesogea Kusini kutoka mpaka wa kaskazini wa Chad na Libya na walikuwa wanasonga mbele kuelekea mji mkuu.

XS
SM
MD
LG