Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Desemba 24, 2024 Local time: 02:37

Tshisekedi aagiza kongamano la amani la Kivu Kusini kulikoathiriwa na migogoro ya kikabila


FILE PHOTO: Tshisekedi, President of Democratic Republic of Congo, attends the Human Rights Council at the United Nations in Geneva
FILE PHOTO: Tshisekedi, President of Democratic Republic of Congo, attends the Human Rights Council at the United Nations in Geneva

Nchini jamhuri ya kidemokrasia ya Congo kumeanzishwa kongamano kubwa kuhusu amani na maendeleo ya Jimbo la Kivu kusini mjini Bukavu.

Kongamano hili litakalo dumu muda wa siku 4 linajumuisha wawakilishi wa makabila mbalimbali toka maeneo tofauti ya jimbo la Kivu kusini.

Kongamano hilo ni agizo la rais wa Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo katika lengo la kujaribu kusitawisha jimbo la Kivu kusini lililoathirika na migogoro ya kikabila pia uongozi mbaya. Linaandaliwa na Jopo Viongozi wa asasi za kiraia ajili ya amani na maendeleo kwakifupi LIPADE, kwa ushirikiano na itifaki ya rais wa jamhuri ya kidemokrasia ya Congo. Joseph Nkinzo ni mratibu wa jopo la viongozi wa asasi za kiraia ajili ya amani na Maendeleo, anaeleza kwa kina umuhimu wa kongamano hili:

"Nadhani kwamba makundi haya yanafanya vita kwa sababu yakukosa maendeleo. Umaskini unasukuma vijana wengi kujiorodhesha katika makundi yenye silaha. Na ikiwa watu hawazungumzi kila mtu anatafuta faida zake mwenyewe kwa njia ya siasa au ya silaha, ila tunapoketi pamoja kama jamii, hii ni njia ya fikra" anasema Joseph Nkinzo , Msimamizi wa Asasi ya Lipade.

Kati ya yanayojadiliwa ni haswa masuala ya uongozi bora, usalama na mshikamano wa kijamii, usimamizi wa ardhi na makubaliano makubwa, utawala wa maendeleo ya kiuchumi na kijamii, utawala wa maliasili na mazingira, Kivu Kusini na mahusiano yake ya kijiografia na kidiplomasia katika ukanda wa maziwa makuu, pamoja na masuala mengine ya kijamii na kitamaduni. Profesa Philippe Kaganda Mulumeoderhwa Doudou anashiriki kongamano hili na anasema "Tuaminiane, hii nayo ni lazima katika uongozi. Watu wanapokutana na kuahidiana bila kutimiza, kesho wanakumbushana ahadi waliofanya”.

Ijapokuwa kuna baadhi ya makongamano yaliyofanyika tangu awali, walioshiriki wakasaini makubaliano na kutangaza maazimio ila muda mfupi baadae kila pendekezo likakiukwa. Akiwa pia msimamizi wa shirika linaloitwa hatua kwa ajili ya maendeleo na amani kwa kifupi ADEPAE, Tharcice Kahayira ni miongoni mwa washiriki toka kabila la Banyamulenge, anahisi kwamba huenda fursa hii itakuwa nzuri Licha ya vikao vingi hivyo, bado tuna haja ya vikao ili kuleta mageuzi kwa watu, na pia kusaidia taasisi kuboresha uongozi” aliongeza.

Profesa Jacques Djoli ni mbunge wa kitaifa mchaguliwa wa jimbo la Tshuapa, akiwa pia naibu kiongozi wa kwanza wa kamisheni ya ulinzi na usalama kwenye bunge la taifa, na hapa ametoa pendekezo “watoto wa Kivu, tuna utajiri wote wa madini, Coltan, dhahabu na kadhalika. Basi tudhamirie kujenga jimbo hili la kivu kusini”alisema.

Kongamano hili pia ni fursa kwa wawakilishi hao wa makaliba mbalimbali kukemea vita katika jimbo jirani la Kivu ya kaskazini na kupongeza juhudi za kuleta amani katika eneo hilo la mashariki mwa Congo, wakidai adhabu kwa wanaozorotesha usalama wa eneo hilo.

Imeandaliwa na Mwandishi wa voa Bukavu Mitima Delachance.

XS
SM
MD
LG