Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Novemba 22, 2024 Local time: 13:36

Wanamgambo wa CODECO wameuwa watu ambao walikuwa wamewateka nyara DRC


Wanamgambo wa kundi la CODECO nchini DRC
Wanamgambo wa kundi la CODECO nchini DRC

Kundi la wanamgambo la CODECO limeua watu 17 ambao liliwateka nyara siku ya Jumamosi katika eneo la Djugu, kiasi cha kilomita 45 kaskazini mwa mji wa Bunia, katika jimbo la Ituri.

Kiongozi wa kijamii katika sehemu hiyo Banguneni Gbalande, ameliambia shirika la habari la Ufaransa AFP kuwa amezijulisha baadhi ya familia za wale waliouawa.

Kundi la wanamgambo ambalo linajulikana kama Cooperative for the Development of the Congo - CODECO, ni moja kati ya makundi kadhaa ya wanamgambo yenye silaha mashariki mwa Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo, ambako kuna utajiri mkubwa wa madini.

Kulingana na mkaazi mmoja wa Bambu, mojawapo ya vijiji viwili vilivyoshambuliwa Jumamosi, kundi hilo liliwateka nyara raia baada ya wapiganaji wake watatu kuuawa na kundi hasimu la wanamgambo.

Kati ya waliotekwa nyara ni mwanamke mja mzito, kilisema chanzo ambacho hakikutaja kutajwa kwasababu za kiusalama.

Karibu kila wiki, Darzeni ya watu wamekuwa wkaiuawa katika mashambulizi yanayofanywa kwenye jimbo lenye utajiri wa dhahabu tangu mwishoni mwa mwaka 2022.

Katika siku za karibuni wapiganaji wa CODECO wameshutumiwa kwa mauaji ya takriban watu 30 wakiwemo wanawake na watoto.

Kundi la wanamgambo la CODECO linadai kuilinda jamii ya walendu kutokana na mashambulizi kutoka kwa jamii nyingine ya wahema pamoja na wanajeshi.

XS
SM
MD
LG