Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 01:22

Mshambuliaji auwa watu 6 katika shule ya jimbo la Marekani la Tennessee


Watoto wa shule ya kikatoliki ya Nashville, Tennessee, wakipelekwa kwenye eneo salama baada ya shambulio la bunduki kwenye shule yao, Machi 27, 2023
Watoto wa shule ya kikatoliki ya Nashville, Tennessee, wakipelekwa kwenye eneo salama baada ya shambulio la bunduki kwenye shule yao, Machi 27, 2023

Mshambuliaji mwanamke Jumatatu aliwaua watoto watatu na watu wazima watatu katika shule ya sekondari ya kikatoliki katika jimbo la kusini mwa Marekani la Tennessee, kulingana na maafisa.

Polisi walimpiga risasi na kumuua mshukiwa, ambaye awali walisema alionekana kuwa kijana. Baadaye maafisa walibaini kuwa mshukiwa alikuwa na umri wa miaka 28 na alikuwa mwanafunzi wa zamani katika shule hiyo.

Msemaji wa idara ya polisi ya Nashville, Don Aaron, alisema mshambuliaji alikuwa na bunduki mbili zinazofyatua risasi nyingi kwa muda mfupi na bunduki moja ya mkononi.

Maafisa hawakumtambulisha mshambuliaji na kusema bado hawajabaini nini ilikuwa nia yake.

Polisi waliwataja waliouawa kuwa wanafunzi watatu na wafanyakazi watatu watu wazima.

XS
SM
MD
LG