Katika Shambulizi hilo mtu huyo pia aliwajeruhi watu wengine tisa katika eneo lake la kazi jana Jumatatu wakati akichukua picha ya video moja kwa moja kwenye mtandao wa kijamii.
Karine Jean Pierre, msemaji wa White House anasema: “ Kwa mara nyingine tena, rais ametoa wito kwa Wa-republican katika bunge kufanya kazi pamoja na Wa-demokrat kuchukua hatua za kupiga marufuku silaha za mashambulizi na zenye uwezo wa juu ili kuwa na hifadhi salama ya silaha , kufanya uchunguzi wa mauzo yote ya bunduki, ili kuondoa kinga kwa watengenezaji wa bunduki. Haya ni mambo ya kawaida ya msingi tunaweza kuuliza na lazima tufanye sasa.
Alisema pia: "Ni kitu Wamarekani wanakitaka, tunajua watu wengi wanaunga mkono hili. Badala yake tunawaangalia maafisa Wa-republican mmoja baada ya mwingine wakipuuza miswaada na hivyo kuzifanya shule zetu, maeneo yetu, sehemu ya ibada, na jamii zetu zisiwe salama sana, Wamarekani wengi wanalipa maisha yao. Kwa hiyo kwa mara nyingine tunabidi tuchukue hatua, tunataka kuona Wa-republican wanaonyesha ujasiri. Warepublican katika bunge.
Mshambuliaji aliuwawa kwa risasi katika eneo la tukio, polisi wa Louisville walisema.
Haijafahamika kama alipigwa risasi na polisi au alijiuwa mwenyewe.
Tukio hilo ni la hivi karibuni kabisa kutokea kuhusu ushambuliaji mashambulizi ya risasi kwa watu wengi marekani.