"Wizara ya Ulinzi inaendelea kukagua na kutathmini uhalali wa nyaraka hizo zilizopigwa picha ambazo zinasambazwa kwenye tovuti za mitandao ya kijamii na zinaonekana kuwa na nyaraka nyeti za siri," naibu msemaji wa Pentagon Sabrina Singh alisema katika taarifa.
Singh alisema usalama wa taifa ni kipaumbele cha hali ya juu sana cha Pentagon na kwamba maafisa wa Marekani "wameshirikiana na washirika na wameziarifu kamati husika zenye mamlaka ya kisheria kuhusu ufichuzi huo."
Wizara ya Sheria ya Marekani ilisema Ijumaa kuwa imefungua uchunguzi kuhusu suala hilo.
Taarifa hizo zinazosambaa, ni pamoja na tathmini za kijeshi kuhusu vita vya Russia nchini Ukraine na washirika wa Marekani, zimeonekana kwenye tovuti mbalimbali za mitandao ya kijamii.
Baadhi ya taarifa ya habari hii imetoka katika mashirika ya habari ya AP na AFP