Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Novemba 22, 2024 Local time: 22:51

Chanzo cha utunzaji wa nyaraka za siri za ofisi ya urais Marekani, na historia yake?


Nyaraka zilizokutwa na wafanyakazi wa Shirika la Upelelezi nchini Marekani FBI katika makazi ya jumba la fahari la Mar-a-Lago la Rais wa zamani Donald Trump' huko Florida.
Nyaraka zilizokutwa na wafanyakazi wa Shirika la Upelelezi nchini Marekani FBI katika makazi ya jumba la fahari la Mar-a-Lago la Rais wa zamani Donald Trump' huko Florida.

Wakati Makamu wa Rais w zamani wa  Marekani Mike Pence amejiunga na kundi la maafisa wa ngazi ya juu waliokiuka utunzaji wa nyaraka za siri.

Marais wa Marekani na makamu wa rais kadhaa kuanzia enzi za Jimmy Carter, amiri jeshi mkuu wa zamani mwenye umri mkubwa kabisa, hivi sasa wanalazimika kujibu uchunguzi wa umma iwapo walifuata taratibu katika kurejesha nyaraka za siri walipoachia madaraka.

Wawakilishi wa rais wa 39 wa Marekani, ambaye alikuwa madarakani kutoka mwaka 1977 hadi 1981, walisema alifanya hivyo.

“Japokuwa Rais Carter hakuwa anawajibika chini ya Sheria ya Kumbukumbu za Urais, ambayo ilianza kutumika baada ya kumalizika muda wake, hata hivyo kwa hiari yake alizikabidhi nyaraka na kumbukumbu zake kwa Hifadhi ya Taifa, baada ya kuondoka madarakani na aliiagiza timu yake kufanya kazi kwa karibu na ofisi ya Hifadhi ya Taifa kuhusu uhamishaji huo,” msemaji mmoja aliijibu Sauti ya Amerika kwa njia ya barua pepe.

Rais wa Marekani wa zamani Jimmy Carter ..
Rais wa Marekani wa zamani Jimmy Carter ..

Sheria ya Kumbukumbu za Rais ya 1978 inatoa muongozo kuhusiana na rekodi rasmi za marais na makamu wake baada ya Januari 1981, na uhamishaji wa umiliki halali wa rekodi hizo kutoka umiliki binafsi kwenda umiliki wa umma chini ya usimamizi wa Hifadhi ya Taifa na Kumbukumbu za Taifa (NARA) .

Kituo cha Carter hakikukana taarifa iliyotolewa na shirika la habari la Associated Press kuwa nyaraka za siri zilizoainishwa zilipatikana nyumbani kwa rais huko Plains, Georgia, ingawa kuna wakati zilirudishwa NARA .

Wawakilishi wa Bill Clinton, George W. Bush na Barack Obama wametoa majibu yanayofanana wakijibu swali la Sauti ya Amerika, wakisema marais hao baada ya kumaliza mihula yao walikabidhi nyaraka za siri NARA na hakuna upekuzi wa ziada uliofanyika. Ofisi ya Obama ikieleza kwenye taarifa ya NARA mwezi Septemba kuwa wamekanusha ripoti ya vyombo vya habari kuwa wakati NARA inahamisha masanduku ya rekodi za rais, hayakuwepo katika ofisi, wakati utawala wa Obama unamaliza muda wake.

Mawakili wa Pence walisema "idadi ndogo" ya hati za siri zilipatikana nyumbani kwake huko Indiana wiki iliyopita. Wakati huo huo aliyekuwa Rais wa zamani wa Marekani Donald Trump na rais Joe Biden wako chini ya uchunguzi mwingine wa mwanasheria maalum anayeangalia jinsi gani walivyokiuka utunzaji wa nyaraka za siri.

Mengi bado hayajulikani kuhusu jinsi, lini, na kwa nini nyaraka hizi hazikushughulikiwa ipasavyo. Hata hivyo , maafisa wengi wa zamani na wataalamu wanasema tatizo hili limeenea.

XS
SM
MD
LG