Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 23, 2024 Local time: 15:55

Wizara ya sheria yasema nyaraka ambazo hazitajumuishwa katika uchunguzi wa jinai wa Trump ni chache


Muonekano wa angani wa nyumba ya Rais wa zamani wa Marekani Donald Trump ya Mar-a-Lago huko Palm Beach Florida. Agosti 15, 2022. REUTERS/Marco Bello.
Muonekano wa angani wa nyumba ya Rais wa zamani wa Marekani Donald Trump ya Mar-a-Lago huko Palm Beach Florida. Agosti 15, 2022. REUTERS/Marco Bello.

Wizara ya Sheria ya Marekani  ilisema Jumatatu kwamba ilipata seti ndogo ya vifaa ambavyo vinaweza kuwa na habari kuhusu namba za binafsi za mawakili wa Rais Donald Trump ambazo zinapaswa kutengwa na uchunguzi wa serikali wa hati za hali ya juu ilizozichukua kutoka nyumbani kwa Trump

Wizara ya Sheria ya Marekani ilisema Jumatatu kwamba ilipata seti ndogo ya vifaa ambavyo vinaweza kuwa na habari kuhusu namba za binafsi za mawakili wa Rais Donald Trump ambazo zinapaswa kutengwa na uchunguzi wa serikali wa hati za hali ya juu ilizozichukua wiki tatu zilizopita kutoka nyumbani kwa Trump huko Florida.

Waendesha mashtaka, katika kesi ya mahakamani huko Florida, walisema watatoa taarifa zaidi katika siku zijazo kuhusu kile walichokipata katika masanduku 20 ya vifaa vya mawakala wa FBI walivyochukua kutoka nyumbani kwa Trump Mar-a-Lago wakati wa upekuzi ulioidhinishwa na mahakama.

Nyaraka zilizochukuliwa katika utafutaji ambao haukutangazwa wa Agosti 8 ni pamoja na majalada 11 yaliyo na viwango tofauti vya usalama wa kitaifa ambayo Trump aliyachukua wakati muhula wake kama rais ulipoisha Januari 20, 2021, badala ya kuziwasilisha kwenye Hifadhi ya Taifa kama inavyotakiwa na sheria ya Marekani.

Mwanasheria Mkuu Merrick Garland aliidhinisha upekuzi huo, na uliidhinishwa na jaji wa mahakama ya serikali kuu huko Florida, baada ya waendesha mashtaka kushuku kwamba Trump hakuwa amerejesha nyaraka zote za siri alizokuwa akishikilia hata baada ya kukabidhi mamia ya kurasa za nyaraka za siri kwenye hifadhi mwezi Januari na Juni.

Hati ya upekuzi inayowaidhinisha mawakala wa FBI kutafuta nyaraka hizo ilisema serikali inachunguza ikiwa sheria za kijasusi na kuzuia haki zilikiukwa.

Lakini chini ya taratibu za haki ya jinai za Marekani, mawasiliano yoyote, maandishi au mazungumzo, ambayo Trump anaweza kuwa na amefanya na mawakili wake yanachukuliwa kuwa yanalindwa kipekee.

XS
SM
MD
LG