Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Novemba 22, 2024 Local time: 17:51

Wizara ya Sheria: Upo ushahidi wa jaribio la kuzuia uchunguzi wa kesi ya nyaraka za Trump


Picha ikionyesha nyaraka zilizowasilishwa mahakamani na Wizara ya Sheria Aug. 30, 2022, na kuondolewa baadhi ya taarifa nyeti na FBI, ikiwa ni picha ya nyaraka zilizokamatwa Aug. 8 wakati FBI wanapekua makazi ya Rais wa zamani Donald Trump, Mar-a-Lago, Florida.
Picha ikionyesha nyaraka zilizowasilishwa mahakamani na Wizara ya Sheria Aug. 30, 2022, na kuondolewa baadhi ya taarifa nyeti na FBI, ikiwa ni picha ya nyaraka zilizokamatwa Aug. 8 wakati FBI wanapekua makazi ya Rais wa zamani Donald Trump, Mar-a-Lago, Florida.

Wizara ya Sheria ya Marekani ilisema Jumanne jioni ilikuwa na  ushahidi ulioonyesha  kulikuwa na  juhudi za kuingilia kati  uchunguzi wa serikali wa  nyaraka za siri zilizokuwa zinashikiliwa na Rais wa zamani Donald Trump katika makazi yake huko Florida.

Mshtaka yaliyofunguliwa mahakamani yalieleza kuwa tangazo la mezi Juni lililotolewa na mwakilishi wa Trump lilisema nyaraka zote za siri zilikuwa zimerejeshwa serikalini, pamoja na taarifa zilizotolewa na wakili wa Trump kuwa nyaraka zote zilizobakia White House zilikuwa zinahifadhiwa katika chumba cha hifadhi.

Wizara ya Sheria ilisema wakili huyo aliwakataza wafanyakazi wa serikali kuangalia kilichokuwa ndani ya maboksi katika chumba hicho cha hifadhi kuthibitisha kuwa kulikuwa hakuna nyaraka za siri katika chumba hicho.

Miezi miwili baadae, Idara ya Upelelezi FBI ilitekeleza amri ya kufanya upekuzi katika eneo hilo, na kuchukua maboksi 33 yaliyokuwa na zaidi ya rekodi za siri 100, ikiwemo baadhi ya hizo zenye siri ya juu kabisa.

Wizara ya Sheria imesema mawakala waligundua baadhi ya nyaraka za siri katika ofisi ya Trump katika jengo lake mapema Agosti wakati wa upekuzi.

Kwa mujibu wa sheria ya Marekani, rekodi za urais ni mali ya serikali na lazima zirejeshwe katika hifadhi ya nyaraka za taifa mara kiongozi anapomaliza muhula wake. Trump aliondoka madarakani Januari mwaka 2021.

Trump amekosoa upekuzi uliofanywa Agosti kama haujawahi kutokea na ulikuwa hauna ulazima wowote, akisema anashirikiana na mashirika ya serikali kuu. Mawakili wake wamemtaka jaji wa serikali kuu kumteua kiongozi maalum kupitia nyaraka hizo zilizokamatwa kuona kama kuna ambazo anastahiki kuwa nazo.

Wizara ya Sheria ilisema katika mawasilisho ya Jumanne kuwa Trump alipewa muda wa kutosha kutekeleza ombi la kurejesha rekodi hizo za serikali, na kuwa timu maalum katika wizara hiyo ilikuwa tayari imekamilisha kazi ya kuchuja nyaraka ambazo alikuwa anastahiki kuwa nazo.

Jaji amepanga kuliangalia ombi la Trump wakati kesi hiyo itakaposikilizwa siku ya Alhamisi.

Baadhi ya taarifa hii imechangiwa na mashirika ya habari ya AP na Reuters.

XS
SM
MD
LG