Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 23, 2024 Local time: 20:26

Mke wa kwanza wa rais wa zamani wa Marekani Donald Trump, afariki

Donald Trump na mke wake wa zamani, Ivana Trump, wakipiga picha nje ya jengo la mahakama mjini New York, baada ya Ivana kula kiapo baada ya kupata uraia wa Marekani, May 1988. Picha ya AP
Donald Trump na mke wake wa zamani, Ivana Trump, wakipiga picha nje ya jengo la mahakama mjini New York, baada ya Ivana kula kiapo baada ya kupata uraia wa Marekani, May 1988. Picha ya AP

Familia ya Donald Trump imesema mke wa rais huyo wa zamani wa Marekani, Ivana Trump alifariki mjini New York akiwa na umri wa miaka 73.

Trump aliandika Alhamisi kwenye mitando ya kijamii kwamba “Nina maskitiko makubwa kuwafahamisha wale wote waliompenda, ambao ni wengi, kwamba Ivana Trump ameaga dunia.”

Trump na mke wake walikuwa wanandoa mashuhuri mjini New York katika miaka ya 1980 na 1990 kabla ya talaka yao ya hadharani, na mbaya, baada ya Donald Trump kukutana na mke wake wa pili, Marla Maples.

Lakini katika miaka ya hivi karibuni, Ivana Trump alikuwa na uhusiano mzuri na mumewe wa zamani. Aliandika katika kitabu chake cha mwaka wa 2017 kwamba walikuwa wakizungumza mara moja kwa wiki.

XS
SM
MD
LG