Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Januari 22, 2025 Local time: 23:45

Wizara ya Sheria yatathmini nyaraka zinazoweza kuwa za siri zilizopatikana Kituo cha Biden


Merrick Garland
Merrick Garland

Wizara ya Sheria inatathmini nyaraka kadhaa zinazoweza kuwa za siri zilizopatikana katika ofisi ya Washington ya taasisi ya zamani ya Rais Joe Biden, White House imesema Jumatatu.

Mwanasheria maalum wa rais Richard Sauber alisema “idadi ndogo ya nyaraka zenye alama ya siri” ziligunduliwa wakati mawakili binafsi wa Biden walipokuwa wanasafisha ofisi za Kituo cha Penn Biden, ambapo rais huyo aliweka ofisi alipomaliza muda wa umakamu wa rais mwaka 2017 hadi kipindi kifupi kabla ya kuanzisha kampeni yake ya urais ya 2020 mwaka 2019. Nyaraka hizo zilipatikana Nov 2, 2022, katika “kabati lililofungwa” ofisini, Sauber alisema.

Sauber alisema mawakili hao mara moja waliifahamisha ofisi ya mwanasheria wa White House, ambaye aliijulisha ofisi ya taifa ya Kumbukumbu na Rekodi – walichukua udhibiti wa nyaraka hizo siku ya pili.

“Tangu kugundulika kwa nyaraka hizo, mawakili binafsi wa rais wametoa ushirikiano na ofisi ya taifa ya kumbukumbu na Wizara ya Sheria katika mchakato wa kuhakikisha kuwa rekodi zozote za utawala wa Obama na Biden zinakuwa inavyostahiki mikononi mwa Hifadhi hiyo,”

Mtu ambaye ana uzoefu na masuala haya lakini hana ruhusa kulizungumzia hili hadharani alisema Mwanasheria Mkuu Merrick Garland alimtaka Mwanasheria wa Wilaya ya Kaskazini ya Illinois John Lausch kupitia suala hilo baada ya ofisi ya Kumbukumbu kulipeleka suala hilo wizarani. John Lausch alichaguliwa na Rais wa zamani Donald Trump katika wadhifa huo.

Ofisi ya taifa ya Kumbukumbu haikujibu mara moja ombi la kutoa maoni Jumatatu. Ujumbe ulitaka maoni kutoka Ofisi ya Mwanasheria wa Marekani huko Chicago halikujibiwa mara moja Jumatatu.

Wizara ya Sheria kwa miezi kadhaa imekuwa ikichunguza nyaraka takriban 300 zilizokuwa zinashikiliwa ambazo zilikuwa na alama ya siri na zilipatikana kutoka katika makazi ya Rais wa zamani Donald Trump huko Florida.

Wakati huo, waendesha mashtaka walisema, wawakilishi wa Trump walikataa maombi ya kurejesha nyaraka kamili za siri na walishindwa kuitikia barua ya wito iliyotumwa kwao ikiwataka wazirejeshe nyaraka hizo.

Chanzo cha habari hii ni shirika la habari la AP.

XS
SM
MD
LG